Tafuta

Vatican News
Zaidi ya watoto 850,000 chini ya umri wa miaka mitano wako hatari ya utapiamlo nchini Mali na zaidi ya milioni moja ya watoto hawaendi shule Zaidi ya watoto 850,000 chini ya umri wa miaka mitano wako hatari ya utapiamlo nchini Mali na zaidi ya milioni moja ya watoto hawaendi shule  

Mali:Wasalesian wahamasisha haki za watoto katika elimu!

Wamisionari wa Mtakatifu John Bosco katika kuhakikisha hali ya watoto na vijana nchini Mali wanapata angalau kiwango cha elimu ya chini ya msingi katika maisha yao wamefungua vituo vya shule ya kuandika na kusoma. Na kwa mujibu wa Unicef, ukosefu wa usalama, watoto wengi hawana fursa ya amani, kujifunza na kukua kwa afya

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Zaidi ya watoto 850,000 chini ya umri wa miaka mitano wako hatari ya utapiamlo wa kutisha nchini Mali na zaidi ya milioni moja ya watoto hawaendi shule ya msima na milioni moja hawakwenda shule ya Sekondari. Ili kuchangia katika suala hili mbele ya dharura, Parokia Katoliki ya Touba yenye vijiji 76, inajikita katika huduma zake  kupitia wamisionari wa Mtakatifu John Bosco (Salesiani ) ili kuhakikisha hali ya watoto na vijana nchini Mali wanapata angalau kiwango cha elimu ya chini ya msingi katika maisha yao.

Kati ya shughuli za kimisionari zilizoanzishwa na wamisionari wa Don Bosko, ni kufungua madarasa 15 kwa ajili ya kutoa huduma ya wasiojua kusoma na  kuandika katika jumuiya mahalia. Wasalesiani wanayo mipango mengine pia ya  mafunzo ya ufundi na taaluma nyingine katika mantiki nyingi na wameweza kuunda hata vituo vidogo vidogo vya michez;kufungua shule ya Sekondari na ujenzi wa mabweni kwa ajili ya kuwakaribisha wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali.

Shughuli hii katika nyanja hiyo ya elimu imewezekana kwa sababu nchi ya Mali ni masikini, kutokana na migogoro, na ukosefu wa elimu ambalo ni janga kubwa linaloendelea na ambalo linajikita ndani ya maisha na makuzi ya watoto. Kwa mujibu wa Unicef, wanasema kwamba, kutokana na ukosefu wa hali ya usalama wa nchini watoto wengi hawana fursa ya kuishi kwa amani, kujifunza na kukua kwa afya nzuri.

Nchi ya Mali ambako miaka hii baada ya kuanza mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo ghasia zinazidi kuongezeka, huku watoto nao wazidi kunyimwa haki zao kama vile chakula, elimu na kuishi. Nchi hiyo ambayo iko ndani ya Ukanda wa Sahel ni kanda kavu ambayo inaigawa jangwa la Sahara. Asilimia 90% ya wakazi ni waislam, na wakristo ni asilimia 5%  nusu yao ndiyo wakatoliki.

Taarifa zinabainsiha kuwa japokuwa wakristo ni wachache, lakini Kanisa Katoliki katika nchi hiyo linaendelea  kuwa hai kwa shughuli muhimu ya amani, umoja, mazungumzo ya kidini na hata kwa njia ya huduma ya mafunzo. Kati ya watu wanaojikita katika juhudi hizi ni Askofu Mkuu Jean Zerbo wa Jimbo Kuu Katoliki Bamako na  ndiye Kardinali wa kwanza wa nchi ya Mali aliyetangazwa na Baba Mtakatifu Francisko kunako Julai 2017.

Mwaka 2017, zaidi ya mashule 650 yalifungwa kwa sabababu ya magaidi waliokuwa wametoa kauli kwamba, hakuna elimu, bali ndiyo uislam . Mwaka jana Maaskofu walikuwa wameelezea juu ya hali ya ukosefu wa usalama katika maeneo mengi ya nchini na kusisitiza kuwa, Mali ni kituo cha makundi ya kijihadi  inayoshambulia mara kwa mara kanda ya Sahel. Hayo yalikuwa yamesema na Padre Edmond Dambele, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Mali.

 

 

 

17 November 2018, 15:20