Tafuta

Kanisa la Amazoni lina ulazima wa kufanya mang'amuzi wa mazungumzo na watu wa asilia ili kuweza kuboresha uelewa mzuri na  ulazima wa uongofu kitaalimungu Kanisa la Amazoni lina ulazima wa kufanya mang'amuzi wa mazungumzo na watu wa asilia ili kuweza kuboresha uelewa mzuri na ulazima wa uongofu kitaalimungu 

Colombia:Watu asilia wamesikika sauti yao wakati wa maandalizi ya Sinodi!

Katika mkutano wa maaskofu nchini Colombia na viongozi wa watu asilia katika maandalizi ya Sinodi ya Amazoni 2019, viongozi wa watu asilia wametoa sauti na kuthibitisha kuwa kipindi kirefu walikuwa wanasubiri mkutano kama huo maana wanahitaji kuliambia Kanisa kuwa nao wanataka wainjilishwe kwa kuzingatia utamaduni wao

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tafakari ya kina na mazungumzo yaliyo wazi kati ya viongozi wa watu asilia na maaskofu nane, wamewezesha kutambua vema mahitaji ya uinjilishaji wa watu wa asilia na kutoa mapendekezo yanayowalenga wao! Ndiyo uthibitisho uliwafikia Shirika la Habari za kimisionari Fides, kwa njia ya Bi Elena Gomez wa Caritas nchini Colombia, mara baada ya mkutano wao wa mwisho kati ya mikutano mitatu iliyofanyika nchini Colombia kwa ajili ya maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu wa Amazoni inayotarajiwa kufanyika 2019 mjini Vatican. Mkutano wao umefanyika huko Puetro Inirida, nchini Colombia.

Viongozi asilia kuwa na shuku ya kusema mahitaji yao

Katika mkutano huo viongozi asilia walisema kuwa ni kipindi kirefu walikuwa wanasubiri mkutano kama huo kwa sababu walikuwa wanahitaji kuliambia Kanisa kuwa, nao wanataka wainjilishwe kwa kuzingatia utamaduni wao, anasema Bi Gomez. Katika mkutano huo ulikabiliana na mapendekezo 34 ya Baraza la Sinodi kwa mujibu wa mtindo wake kwa: “kutazama”, “kung'amua” na “kutenda”. Majibu waliyoyapata yameweza kuangalia vigezo vya hali katika kumbukumbu ya uwepo wa Kanisa na mchango wake wa kukabiliana ma matatizo na kilio cha wakazi wa eneo ambalo linajikita katika hali halisi na maalumu kijiografia linalotazama na kuhitaji Kanisa.

Katika mkutano huo, mada tatu msingi zimezingatiwa, ikiwa ni: “uzalendo na kilio cha Panamazoni”; “Kuelekea katika wongofu wa kichungaji na ekolojia ambayo imefunguka kutangaza Yesu katika ukuu wa kibiblia, kitaalimungu, kijamii, kiekolojia, kisakramenti na kimisionari”; “Njia mpya za Kanisa linalotaka kuelekea Amazoni.

Kuna umuhimu wa kutambua watu wa asilia kama wadau wa kwanza kusikilizwa

Bi Gomez akifafanua amasema:Kuna haja ya utambuzi wa watu asilia kama wadau wa kwanza wa kusikilizwa na Kanisa linatambua kwa kikamilifu tasaufi nzima inayojikita ndani ya mzizi ya asili na katika maeneo yao, ambapo watu wa asilia wanashirikishana imani ya mungu mmoja. Hata hivyo akiongeza amethibitisha kuwa, tasaufi hizi za kushirikishana zimewezesha kutoa hitimisho ambalo linasema kwamba utamadunisho daima umekuwa unaeleweka kama mtindo wenye kuwa na makosa. Lakini kumbe “utamadunisho huo hauna maana ya kutazama ishara zipi za imani ya kikristo zilizopo katika tasaufi ya mababu asilia, badala yake,  hilo ni zoezi la maelekezo na  ili watu wa asilia waweze kutambua kwamba, ndani ya tasaufi yao kuna mbegu ya Mungu katika imani ya kikristo na Kanisa kwa upande wake, linatoa kipaumbele katika ngazi ya kiliturujia na kitaalimungu, nafasi ya kujieleza katika tasaufi hiyo”.

mapendekezo yamewekwa ili kupanua ushiriki wa kikundi cha Mafunzo na mitindo ya kichungaji

Kadhalika Bi Gomez ameeleza kuwa katika mkutano huo, wamesema kwamba hiyo inahitaji kwa dhati kuzungumza juu ya utamadunisho. Kanisa la Amazoni lina ulazima wa kufanya mang'amuzi kwa msingi wa mazungumzo na watu wa asilia ili kuweza kuboresha uelewa mzuri na ulazima wa uongofu kitaalimungu, kichungaji, kiekoloja na kiliturujia kwa mujibu wa mapendekezo ya Waraka wa Laudato Si. Na kutokana na hilo, ndipo mapendekezo yamewekwa ili kupanua ushiriki wa kikundi cha Mafunzo na mitindo ya kichungaji, ambayo si tu kuwhusu wanataalimungu, bali pia hata kwa wale wenye hekima na waliopo katika watu asilia!

12 November 2018, 14:31