Tafuta

Vatican News
milioni mbili ya wapalestina wanaishi kama wafungwa karibia miaka 10 sasa katika eneo la Gaza milioni mbili ya wapalestina wanaishi kama wafungwa karibia miaka 10 sasa katika eneo la Gaza  (ANSA)

Ask.Mkuu Pizzaballa:wakristo wa Gaza hawapotezi matumaini!

Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Kilatino mjini Yerusalemu, hivi karibuni alitembelea mpaka wa Gaza kushirikishana mateso na matumaini wakazi wa Kipalestina katika eneo hilo, wakiishi kama wafugwa karibia miaka 10

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

“Ni ziara yangu ya pili huko Gaza na ilikuwa safari yenye ufanisa hasa wa kutaka kuelewa vema hali halisi mahalia. Kwa dhati imekuwa ni fursa nzuri  na zaidi ili kukutana na jumuiya ya Gaza na  kufanya uzoefu nao hali halisi ya  mahangaiko, lakini hata na matumaini”. Huu ni uthibitisho shirika la habari za kimisionari Fides, wa maneno ya Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi wa Kitume wa Upatriaki wa Kilatino mjini Yerusalemu, mara baada ya kutembelea mpaka wa Gaza, eneo ambalo wanaishi karibia milioni mbili ya Wapalestina.

Kushirikishana kipindi cha pamoja na familia ya wenye kuhitaji

Hii ni ziara iliyoanza tarehe 1-4 Novemba 2018 na ambayo yeye mwenyewe anathibitisha kuwa imekuwa fursa kukutana na hali halisi ya jumuiya ya kikristo iliyopo katika eneo hilo (kama vile shule, shughuli za kujamii, scout na makundi ya vijana) lakini pia  kuweza kushirikishana kipindi cha pamoja na familia za wenye kuhitaji. Kadhalika Askofu Mkuu Pizzaballa ameweza kujionea mwenyewe moja kwa moja matatizo ambayo watu wa Gaza wanakabiliana nayo katika kuishi katika eneo hili yenye kufungwa kwa mipaka ya kuvuka kwa watu katika mstari wa Gaza na bidhaa na matatizo mengine mengi ya uchumi na kijamii yaliyopo!

Jumuiya ya kikiristo ya Gaza imeungana

Anakiri kwamba ameweze kuona jumuiya ya Kikristo ya Gaza ilivyobaki imeungana kwa pamoja licha ya kukabiliana na halisi iliyopo na ngumu: “kwa hakina yapo masuala yaliyofunguliwa,lakini tendo la kukutana nao kwa upande wangu limenitia moyo”, anathibitisha. Katika fursa ya ziara yake Askofu Mkuu ameweza kuzindua nyumba kwa ajili ya wazee na walemavu. Na kwa mujibu wa Paroko wa Gaza, padre Mario Da Silva amaesema, zaidi ya uzinduzi wa nyumba mpya pia alikutana na familia za wakristo na waislam. Askofu Mkuu Piazzaballa alihitimisha ziara yake kwa kuadhimisha Misa Takatifu katika Parokia ya Kilatino ya Familia Takatifu, ambalo ndiyo Kanisa pekee lililopo katika mpaka wa eneo hilo na  lenye kuwa na idadi ya  wakatoliki 140 tu.

Milioni mbili ya wapalestina ambao wanaishi kama wafungwa karibia miaka 10 sasa

Taarifa inathibitisha kuwa katika wiki mbili za mwisho, iliibuka mivutano kwa upya kati ya Israeli na wakazi wa Kipalestina wa Gaza, mahali ambapo wachambuaji kwa upande wa kibinadamu na kisiasa, wanasema hali hii siyo nzuri kutokana na milioni mbili ya wapalestina ambao wanaishi kama wafungwa karibia miaka 10 sasa na katika eneno taktribani ya km 400 za mraba wa ardhi.

12 November 2018, 14:57