Baraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki Amecea Baraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki Amecea 

Amecea:warsha kwa wahudumu wa mawasiliano na wakurugenzi

Imefanyika warsha kwa ajili ya wahudumu wa mawasiliano kijamii na wakurugenzi wa kichungaji ili kuweza kukuza ufahamu kuhusu hatari za ulimwengu wa digitali kwa kuzingatia ulinzi wa watoto na vijana dhidi ya unyanyasaji katika mitandao. Warsha hiyo imefanyika mjini Nairobi, Kenya kuanzia 19-23 Novemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wahudumu wa Mawasiliano ya Taifa, Kijamii na Wakurugenzi wa kichungaji kutoka nchi za ya Baraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) wameamua kufanya kazi pamoja ili kukuza ufahamu zaidi kuhusu hatari katika ulimwengu wa digitali, hasa kwa kuzingatia suala la kuzuia na kulinda hadhi ya watoto na vijana dhidi ya unyanyasaji, unyanyasaji kijinsia na matokeo mengi kufuatana na matumizi mabaya, pia na kueneza kwa itikadi mbaya na biashara mtandaoni.

Warsha hiyo imeandaliwa na AMECEA, mjini Nairobi Kenya kuanzia tarehe 19 hadi 23 Novemba 2018 ambapo msingi wake ulikuwa kama utekelezaji wa Mpango wa Mkutano wa Dunia juu ya Hadhi ya Watoto katika Ulimwengu wa Digitali, uliofanyika mjini Roma mwaka 2017. Katika mkutano huo ulitambua haja ya majadiliano ya kimataifa na uelewa wa hatua madhubuti ya kukabiliana na tatizo hilo, linalozidi kuenea kwa kasi na kuwa vitisho vinavyotokana na teknolojia mpya za vyombo vya habari na mtandao, kama vile unyanyasaji wa habari na vitisho, picha za unyanyasaji wa kijinsia zinazoenea mtandaoni; biashara za mitandaoni na katika uhalifu wa kueneza itikadi kali.

Utekelezaji wa Mpango wa Mkutano wa dunia juu ya hadhi ya watoto katika dunia ya digitali

Kufuatia nan a utekelezaji huo ikumbukwe kwamba kuanzia tarehe 3-6 Octoba 2017 ulifanyika  Mkutano wa Kimataifa kuhusu, “Hadhi ya mtoto katika dunia ya digitali, ulioandaliwa na Kituo cha Ulinzi wa Watoto katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana mjini Roma. Katika mkutano huo walithibitisha kuwa watoto na vijana wanaunda robo 3.2 ya bilioni ya watumiaji wa internet duniani. Kizazi hiki cha vijana ni zaidi ya milioni 800 ambao wanaonekana kushambuliwa na hatari ya kuwaathiri kutokana na matumizi mabaya ya digitali, pia matumizi hayo kuwa chanzo cha mambo ya hovyo na yasiyo ya kimaadili; kushuka kwa maadili na unyanyasaji wa kijinsia kwenye huduma ya mawasiliano na mitandao ya kijamii.

Wajumbe wa Kongamano la Kimataifa kuhusu ulinzi wa watoto wadogo kwenye “ulimwengu wa digitali”, lililokuwa linaongozwa na kauli mbiu “Utu wa watoto wadogo katika ulimwengu wa digitali,waliweza kukutana na Baba Mtakatifu  Francisko tarehe 6 Oktoba 2017 pamoja na kumkabidhi “Tamko la Roma” kuhusu ulinzi wa watoto wadogo kwenye “ulimwengu wa digitali. Katika fursa hiyo, Baba Mtakatifu aliwataka wajumbe hawa kuwa makini ili watu wasitumbukie katika mawazo potofu ya kudharau madhara ya nyanyaso za kijinsia wanayofanyiwa watoto wadogo na kuona kuwa ni jambo la kawaida. Kadhalika alisema kuwa, suluhisho la matatizo na changamoto hii si ya kiufundi na inayokuja tu kama maji kwenye glasi, kwa sababu hili ni tatizo lenye utata mkubwa. Na pia akasisitiza kuwa, ni tatizo linaloweza kuwatumbukiza watu katika mtazamo wa kisiasa zaidi kwa kujikita katika uhuru usiokuwa na mipaka unao athiri ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Licha ya manufaa makubwa ya mitandao

Katika Tamko la Roma waliloliandaa linasema maisha ya kila mtoto ni ya pekee, ni muhimu na yana thamani kubwa na kwamba, kila mtoto anapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake pamoja na kupewa ulinzi na usalama. Lakini, leo hii kuna mamilioni ya watoto ambao hawana ulinzi na usalama. Maendeleo makubwa ya teknolojia na matumizi yake katika maisha ya kila siku yanaendelea kuleta mabadiliko makubwa si tu kwa kile ambacho watu wanatenda, bali hata katika utambulisho wao na kwamba, hii ni baraka kubwa. Lakini, kwa upande mwingine, maendeleo haya yameibua giza katika bahari ya ya mitandao ya kijamii ambayo inaacha madhara makubwa kwa ustawi na makuzi ya watoto wadogo.

Mitandao ya kijamii ina manufaa makubwa kwa jamii na ni fursa inayowashirikisha watu ndani ya jamii na kwamba, inatoa nafasi pia kwa watu kujipatia ufahamu wa mambo mbali mbali. Mitandao hii imesababisha kumong’onyoka kwa utu wa binadamu kutokana na madhara yake kwa watoto. Kumekuwepo na ukatili dhidi ya watoto wadogo; nyanyaso za kijinsia na mielekeo tenge ya tendo la ndoa; mambo ambayo kwa sasa yanaonekana kuwa ni ya kawaida hata kwa watoto. Nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo katika mitandao ni tatizo linalotisha sana! Kuna idadi kubwa za picha za ngono walizopigwa watoto na vijana na zimesambazwa kwenye mitandao ya kijami na zinaendelea kuongezeka maradufu.

Katika warsha la AMECEA linabainisha mapungufu katika eneo mahalia

Kutokana  Tamko hilo, ndipo warsha   la  AMECEA  limeweza kubainisha mapungufu yafuatayo na mhalia kama mambo ya hatari ambayo yanapaswa kushughulikiwa katika mazingira ya ulinzi wa watoto kwa kulindwa kutokana na matumizi mabaya  mtandaoni:kwanza ukosefu wa ufahamu juu ya hatari ya matumizi ya internet kati ya watoto wengi, vijana na umma kwa ujumla mahalia; Kanisa katika eneo hilo halikatai juu ya ukweli wa matukio ya unyanyasaji wa watoto yanayotoke, japokuwa ni kutokana na  ukweli kwamba hakuna utafiti juu ya kesi za unyanyasaji wa watoto uliofanywa katika nchi yoyote ya AMECEA na kwamba kile kinachotoka wanakipata kutoka katika ripoti za mara kwa mara za vyombo vya habari vya umma. Vikwazo vingine vinavyotambuliwa ni pamoja na ukosefu wa mafunzo sahihi kutoka kwa wahusika wa Chama cha Kipapa cha kimisionari (PMS) mahalia; Ukosefu wa Sera za ICT kuhusu ulinzi na kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji na matumizi ya mtandaoni; ukosefu wa ufahamu kuhusu kanuni za Serikali juu ya mantiki za mtandao na ukosefu wa  wa miundo sahihi ya Kanisa na Serikali kushughulikia maswala ya unyanyasaji wa watoto kati ya wengine.

Kwa kutumia vyombo vya habari na warsha, ili kuhamasisha uwelewa zaidi

Washiriki wa warsha hiyo wameamua kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na uelewa zaidi kupitia matumizi ya vyombo vya habari,semina na warsha, harakati za ndani, za kushawishi ili kuweza kuingizwa kwa sera zinazohusu ulinzi wa watoto katika mitaala ya masomo shuleni kuanzia na taasisi Katoliki na uwezekano wa kuleta majadiliano katika  jumuiya ndogo ndogo za kikristo  na makundi mengine ya kile ambayo ni vya vya kitume. Hata hivyo taarifa zinathibitisha kuwa:Warsha hiyo imefanikiwa kutokana na msaada wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani ambao wanachangia kwa sehemu kubwa ya mpango huo.

29 November 2018, 14:32