Tafuta

Vatican News
Kuna haja ya kuendelea kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake,kufuatia na kumbukumbu ya siku hiyo inayofanyika  kila mwaka ifikapo tarehe 25 mwezi Novemba Kuna haja ya kuendelea kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake,kufuatia na kumbukumbu ya siku hiyo inayofanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 mwezi Novemba  (ANSA)

Kard. Bassetti:mwanamke ni chanzo cha chemi chemi ya maisha!

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, kwa njia ya Video Kardinali Bassetti anawaalika watu waeneze picha ya Bikira Maria mwenye jicho jeusi, ishara ya mwanamke aliyekiukwa utu wake

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Rais wa Baraza la Maaskofu Italia, Kardinali Gualtiero Bassetti ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kupitia Luninga ya Baraza hilo, kufuatia na maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, ambayo inafanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 mwezi Novemba.  Kardinali Bassetti katika ujumbe wake anasema:Wale wanaomtendea vibaya mwanamke ni kukataa na kushindwa kutambua mizizi yao kwa sababu wanawake ni chanzo na chemi chemi ya uzazi. Ni aina ya kukufuru kumwua mwanamke. Vurugu dhidi ya wanawake inazidi kuwa dharura hata katika ngazi ya kitaifa ambayo inapaswa kupambananaya  hata katika ngazi mbalimbali anathibitisha.

Akiendelea na ujumbe wake, Kardinali Bassetti anataja uzoefu ake kama  Mchungaji, ya kwamba amekutana na hali halisi ya kweli na ya kutia wasiwasi. Wanawake wengi wamekwenda kwake kwa faragha pia kwa aibu wakiogopa iwapo wanaweza wasiaminiwe kile anachokitoa au wenza wao wakitambua kuwa wameshitakiwa, kwa maana hiyo Kardinali anathibitisha kwamba, hiyo ni mbaya kwa sababu imani yao ambayo ingeweza kuwasaidia, inabakia bila kupata jibu sahihi.

Manyanyaso juu ya wengine

Kardinali anatoa swali: Je ni jinsi gani ya kuelezea, mwanaume ambaye kwa nje anaoneka ni mtu mwema na mzalendo na kumbe baada ya kuingia ndani ya kuta za nyumba anageuka mkatili?  Hata hivyo amebainisha Kardinali kuwa: “Mara nyingi wanawake wanashindwa kutambua vurugu na tendo la upendo, kwa sababu, wengine wanasema, iwapo ananipiga, au kunipiga kofi, ni kwa sababu ananipenda, ina maana ya kuwa na wivu nami, na kwa maana hiyo anatakia mema”. Kardinali Bassetti anaongeza kusema: “Kutokana na hili, kuna wengine wanajinyenyekeza kwa sababu ya upendo.  Lakiniu hiyo ni wazi kwamba hayo yote hayawezi kujionesha katika upendo wa kwel,i bali ni maonesho ya kutaka kutawala kwa mabavu na vurugu na pia  manyanyaso juu ya mwingine”.

Wosia wa Amoris laetitia ni wenye hekima

Kardinali Bassetti akiendelea kutoa ujumbe wake kwa njia ya video anasema, Baba Mtakatifu Francisko ametoa ujume wake ulio wazi na hekima unapotikana katika Wosiwa wake wa Amoris laetitia kwamba: “Vurugu ya aibu ambayo wakati mwingine hutumiwa dhidi ya wanawake, unyanyasaji wa ndani ya familia na aina mbalimbali za utumwa sio maonesho ya nguvu za kiume, bali ni udhaifu na  kuondoa heshima”. Vurugu na kuwekea vikwazo vya maneno, unyanyasaji wa kimwili na kijinsia dhidi ya wanawake hupingana na asili ya umoja wa ndoa. Ni muhimu kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Kardinali Baasseti pia ametaka kuzungumza kwa nguvu zote ya kwamba: “kwanza kabisa katika mtazamo wa kiutamaduni, akiimanisha kambi ya kwanza ambayo inapaswa kuhusika ni elimu kuanzia katika mashule, na katika yale ambayo ametaja yanaitwa mashirika ya elimu, familia na mantiki zote za ubunifu na burudani. Akitoa mfano amesema wakati mwingine hata katika mchezo, mahali ambapo panapaswa pawe na mtindo wa elimu, lakini panajitokeza mitindo ya vurugu. Kila aina ya vurugu inayojitokeza katika udogo, na baadaye inazidi kukua kwa kuumiza mwingine aliye jirani.

Ukaribu wa Kanisa kusaidia wanawake waathirika wa vurugu

Katika juhudi za kupambana, Kardinali Basseti, anasema: “Kanisa kwa nguvu zote na jitihada zake liko mstari wa mbele katika karibu kwasaidia wanawake waathirika wa vurugu na nyanyaso. Na kama makuhani mara nyingi wanatakiwa kukaa kwa dhati kusikiliza simulizi kwa yule anayethirika na vurugu hizo. Lakini kuna ulazima wa  kuwa wakarimu, makini na kuhepuka haraka haraka mbele yao. Anaongeza ninasema hivyo kwasababu ninao utambuzi na furaha ya kwamba, kuna majimbo kuanzia na Roma ambayo yanajikita kufungua milango yao ya ili kusikiliza na kusaidia wanawake wote wenye matatizo,  hata kwa ajili ya watoto wao. Hiyo ni kwa sababu hatupaswi kusahau kuwa mahali penye mwanamke anayeathirika, mara nyingi wapo wadogo wasio kuwa na hati na ambao wanalazimika kuona vurugu hizi. Je ni mfano gani tunawapatia watoto wetu? Kardinali anauliza swali hili.

Picha ya Bikira Maria mwenye jicho jeusi

Kardinali Bassetti anahitimisha kwa kutazama picha ya Bikira Maria iliyechorwa enzi za miaka ya 600 ambayo inaonesha jicho jeusi. Picha hii inahifadhiwa katika Madhabahu ya Bikira Maria huko Galatone wilaya ya Lecce nchini Italia. Historia tyake ni kwamba mwanamme mmoja alirusha jiwe na kuidhuru picha hiyo katika mboni ya jicho la kulia. Mara moja baada ya tendo hilo, katika mzunguko wa jicho ulitokea oshara  fulani inayoonesha kuumia kwa jicho hili hadi sasa. Ni picha ambyao inatafsiria kuwa ishara ya vurugu dhidi ya wanawake.

Kutokana na hiyo picha, Kardinali Bassetti amesema: “Ni picha nzuri sana ambayo mimi sikuwa ninaifahamu, ni bora kuineza” ni picha ya Maria iliyokiukwa  na kutoheshimiwa. Na hii picha ya Maria iliyokiukwa katika uso wake mzuri ni picha inayoonesha kwa karibu jinsi gani ya kukufuru na vurugu zinazotendewa mwanamke. Na kwa sababu hiyo, kila mwanamke awe ni mdogo au mzee daima ni dada na mama wa kuheshimu. Na yeyote asiyemheshimu mwanamke, haheshimu mizizi yake na haheshimu maisha”. Kardinali Bassetti amethibitisha.

26 November 2018, 15:20