Cerca

Vatican News
Maaskofu nchini Chad Maaskofu nchini Chad 

CHAD:mamilioni ya watu katika ziwa la Chad wako hatarini!

Tangu mwaka 1960 hadi sasa kwa dhati ziwa Chad limezidi kupungua kwa kiasi cha asilimia 90%, na wakati maisha endelevu ya kila siku ya watu yanategemea ziwa hilo. Huo ni uthibitisho kutoka kwa mwakilishi wa Caritas kanda ya kaskazini nchini Chad

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Inahitaji kuwekeza kiasi cha kweli  hasa katika  matukio yanayojumuisha jumuiya mahalia. Katika mchezo huo kuna mamilioni ya watu  ambao ndiyo wa wakati endelevu na ambao maisha yao kila siku yako katika uzi wa njia mbili kuelekea ziwa Chad”. Ndiyo uthibitisho wa Edouard Kaldapa, Mkurugenzi wa Caritas wa Marua- Mikolo wa Kanda ya ncha ya kaskazini, inayopakana na nchi ya Camerun, pia kupakana na Nigeria  na Chad hadi ukingo wa Ziwa Chad, mahali ambapo watu mahalia ni waathirika kwa kipeo cha mazingira. Tangu mwaka 1960 hadi sasa kwa dhati eneo hilo la ziwa limezidi kupungua kwa kiasi cha asilimia 90%.

Milioni 19 ya watu katika kipeo cha ziwa Chad

Akifafanua Kaldapa katika vyombo vya habari katoliki Sir, amethibitisha kuwa: “Kwa sasa, wapo watu milioni 19 waliokumbwa na kipeo hicho na iwapo hali hiyo itazidi kuendelea,  itakuwa ni janga kubwa. Ziwa linawakilisha kama kizingiti cha mwisho dhidi ya jangwa lililopo na ambalo ni kisima cha maisha kwa ajili ya milioni arobaini ya  watu.

Hata hivyo Taarifa zinasema kuwa, Mkurugenzi huyo wa Caritas, ameshiriki hivi karibuni katika Mkutano wa ngazi ya  juu , ulikuwa inahusu kanda ya mto Chad,mkutano  uliofanyika mjini Berlin Ujerumani.  Caritas nchi Ujerumani, ilikaribisha mkutano huo, ambapo pamoja na mkurugenzi huyo, walikuwepo wawakilishi wengine 24 kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa, wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Bank ya dunia, Bank ya maendeleo Afrika na nchi nyingine ishirini na saba, zikiwemo nchi zote nne zinazopakana na ziwa Chad (Camerun, Chad, Niger na Nigeria).

Suluhisho la kipeo cha ziwa Chad

Wawakilishi wote hao wameitwa kukabiliana na suala msingi hasa  juu ya uwezekano wa kutafuta suluhisho la kuzuia kuendelea kukumbwa kwa eneo hilo la ziwa. Mkutano huo ulihitimishwa kwa kujiwekea mkakati wa juhudi ya kufanya hasa kwa kuwekeza bilioni 2,77 dola za  kimarekani, ili kuboresha hali halisi ya jumuiya mahalia: na nchini Italia itachangia euro milioni kumi na tano mwaka 2019.

16 October 2018, 13:42