Cerca

Vatican News
Chama cha Kanisa Hitaji kinahamasisha watoto kusali Rosari kwa ajili ya amani na umoja duniani Chama cha Kanisa Hitaji kinahamasisha watoto kusali Rosari kwa ajili ya amani na umoja duniani 

Watoto duniani kote wanaombwa kusali rosari tarehe 18 Oktoba!

Tarehe 18 Oktoba, Chama cha Kanisa Hitaji linawaalikwa watoto wote duniani kusali. Ni milioni moja ya watoto wanasari Rosari pamoja kwa ajili kuomba umoja na amani. Na huo ni mwendelezo wa maombi ambayo yameanza tangu miaka 13 iliyopita

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 18 Oktoba, Chama cha Kanisa Hitaji linawaalikwa watoto wote duniani kusali Rosari kwa ajili ya kuombe umoaj na amani duniani. Hayo ni mapendekezo ambayo kwa miaka 13 iliyopitia imeweza kuwakusanya watoto wengi katika kusali pamoja. Wanashiriki hadi sasa wa watoto ni karibia wa nchi 80  kutoka mabara yote duniani. Anathibitisha hayp Padre Martin Barta, Mhusika wa Kanisa Kimataifa wa Chama cha Kanisa Hitaji. “Mwaka jana hata nchi ya Argentina, Cuba, Cameruni, India, hadi Ufilippini ziliweza kushiriki, na kwa dhati ni tukio katika Kanisa lote duniani”amaesisitiza.

Barua ya kuwaalika watoto na watu wote kusali Rosari

Katika mitandao ya kijamii wameweze kutoa mwongozo wa kusali Rosari, zana zinazo hitajika, hata barua kwa ajili ya watoto na watu wazima, barua iliyotafsiriwa katika lugha 25, kama vile kiarabu, au kiausa na lugha nyingine nyingi. Padre Barta akifafanua, amesema utume wa sala ulianzishwa kunako mwaka 2005 huko Caracas nchini Venezuela. Wakati kikundi cha watoto wakisali karibu na duka moja na baadhi ya wanawake waliokuwapo, walihisi uwepo wa Bikira Maria.

Mmojawapo kati yao akikumbuka ahadi ya Padre Pio kuwa: “Iwapo milioni mija ya watoto watasali pamoja Rosari, dunia itabadilika.” Na ndiyo kwa dhati, Padre Baerta anasisitiza kwamba, ni matumaini yake aliyo nayo ya nguvu ya sala ya watoto.  Yesu anatufundisha: “iwapo hamtageuka kama watoto , hamtaingia katika ufalme wa Mungu” ( Mt 18,3).

Sikukuu ya Mtakatifu Luka Mwinjili

Tarehe 18 Oktoba ilichaguliwa kutokana na kwamba ni katika mwezi wa Maria  lakiniwakati huo huo,  siku hiyo Mama Kanisa anakumbuka Sikukuu ya Mtakatifu Luka mwinjili. Mtakatifu Luka, amerithisha kizazi hadi kizazi historia ya utoto wa Yesu,na kwa mujibu wa  mapoke ya utamaduni, yeye alikuwa na uhusiano mkubwa na Maria  Mama wa Mungu na kwa maana hiyo tarehe hii ni mwafaka.

Chama cha Kanisa Hitaji daima kinaunganisha msaada wa kichungaji wa Kanisa duniani kote,  hata kutangaza na kupinga vikali vikwazo vilivyopo dhidi ya uhuru wa kidini na ambo ndiyo msingi wa kuanzisha kwa ala hiyo.

Padre Barta anasisitiza kwamba, wao wanahisi kuwa ndani ya  jumuiya ya Kanisa , ambayo ina kazi hiyo ya kujikita kila siku katika nchi 149 duniani kote.

Ni Mungu peke yake aweza kuleta amani

Chama cha Kanisa hitaji kinafanya uzoefu wake wa kikristo katika dunia ambayo inateseka sana kwa sababu ya ubaya na vurugu za vita. Ni mungu peke yake anaweza kuleta amani. Jambo ambalo wao wanaweza kufanya ni kuchangia katika kazi yao, lakini zaidi ni katika kusali.

Kutokana na hilo kwa njia ya makao 23 katika mataifa mbalimbali, Chama cha Kanisa Hitaji kinawaalika wazazi, walimu na wote wanaohusika katika mashule ya ngazi zote, hospitali, vituo vya watoto yatima na kila aina ya sehemu ambayo kuna vikundi vya watoto kuwahamasisha wadogo wasali Rosari duniani kote kwa ajili ya kuomba amani.

 

11 October 2018, 15:43