Tafuta

Wasiwasi wa maaskofu wa Honduras juu ya utunzaji wa mazingira Wasiwasi wa maaskofu wa Honduras juu ya utunzaji wa mazingira 

Hunduras: Maaskofu wana wasiwasi kuhusu mazingira!

Katika waraka wa mwisho wa Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa Honduras uliohitimishwa hivi karibuni, maaskofu na wadau wa sekta ya utetezi wa mazingira, wanaonesha wasiwasi mkubwa juu ya hali ya migogoro ya viwanda inayozidi kunyonya rasilimali ya asili

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maaskofu wa Honduras pamoja na sekta za watu wanaojikita katika utetezi na ulinzi wa mazingira, wanatazama kwa wasiwasi mkubwa juu viwanda katika migogoro ya mazingira ambayo yamezidi kunyonya rasilimali ya asili. Ni maneno yaliyomo katika ujumbe wa mwisho wa Mkutano wa Baraza la Maaskofu uliotolewa kwa vyombo vya habari mara baada ya mkutano huo hivi karibuni.

Waraka huo unachukua  mada  hiyo kutokana mafuriko ya hivi karibuni, ambayo yaliikumba nchi na kusababisha  maafa mengi ambayo ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi, lakini pia hata matumizi mabaya ya sera za mazingira, ambayo bado yanazidi kushambuliwa kwa namna ya kutowajibika. Matukio haya huko Hunduras, Amerika ya Kusini, inajionesha hasa katika sekta ya madini ambayo imekuwa ni sehemu ya kunyonywa, kutokana na migogoro ya kijamii na mfumo mzima wa jumuiya mahalia.

Uwajibikaji wa makampuni ya kuchimba madini na viongozi wa raia

“Utekelezaji mbaya wa sheria, pamoja na hali mbaya ya sheria iliyowekwa pia udhaifu wa sherikali yao, maaskofu wanasema, imewewza kuweka katika  nchi yao makubaliano ya madini na umeme bila kutekeleza sheria, ambazo zinapewa maeneo ya hifadhi katika mbuga  za taifa, na wakati huo watu  walioathirika, hawaulizwi kabla ya kufungua maeneo mapya ya madini, kama inavyotakiwa na ilivyo andikwa sheria ya nchi”.

Maaskofu wanaendelea kuthibitisha kuwa, “Hii ni kukidhi wawekezaji wasio na uaminifu na wajasiriamali wasio na dhamiri ya kijamii”  Suala hili  pia kinatazama haya kuangalia suala la ubinafsi kibinadamu na ukosefu wa upendo wa utaifa kwa viongozi wa umma ambao wanawahukumu watu kwamba ni wahalifu wakati wananunua ukimya au vyombo vya habari za kugushi”.

Kuhamasisha mtindo wa maendelo fungamani ya watu

Wakikumbuka mafundisho jamii ya Kanisa, kwa namna ya pekee maneno ya Papa Francisko ya Waraka wa Laudato Si, kuhusu utunzaji wa mazingira nyumba yetu, maaskofu wanaomba ufuatwe mtindo wa dhati wa  maendeleo fungamani ya watu  ambao unakwenda moja kwa moja katika mazingira endelevu na kuheshimu haki za binadamu.

Na hatimaye kutokana na suala la utunzaji bora wa mazingiria, ndipo maaskofu wanatoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuimarisha kwa  upya haki, sheria, uhalali na amani, na kwamba ni matumaini yao, migogoro inayoendelea nchini mwao inaweza  kutatuliwa kwa amani na kwa njia ya  mazungumzo.

17 October 2018, 15:51