Tafuta

Vatican News
2016-08-04 Papa Francesco in visita pastorale ad Assisi

Tusiwe na Kanisa kavu na lenye kutaka kujitosheleza!

Kardinali Stella ameonesha njia mbili pendelevu za kukutana na Kristu, kwa upande wa vijana:Neno la Mungu na Liturujia. Kwa hiyo, ni kwa namna gani vijana wa leo wataweza kukutana na Yesu, katika “kuona uso wake, kuacha kuulizwa Naye na kumfuata kwa furaha”, ni katika kipimo ambacho “ tutawasidia kuishi uzoefu wa mahusiano haya na Yesu kwa kupitia Neno la Mungu”.

Sr. Angela Rwezaula na Frt. Emily Sibomana - Vatican

“Tunatakiwa kukubali kuwa picha ya Kanisa ambayo tumewapa vijana  na mtindo ambao umechukuliwa umbo katika kuonesha imani kwa wakristo wengi, siyo daima kuwa imewakilishwa katika njia inayoelekeza kukutana na Bwana, na uzuri wa Ukristo”. Hayo yamesisitizwa na Kardinali Beniamino Stella, Rais wa Baraza la kipapa la Makleri, wakati wa kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa 22 kuhusu "utafiti wa sura ya Kristo". Ni mkutano uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Urbaniana kuanzia tarehe 29-30 Septemba 2018.

Hapana kuwa na kanisa kavu na lenye kujitosheleza

Mara kadhaa, nafasi ya Kanisani imetoa mkazo wa kuwa sehemu pekee na muhimu”, ameongeza Kardinale Stella, ambapo mkazo mkubwa “ katika kufuata sheria umefifisha mtetemo usiotabilika wa neema. Cha zaidi, uhitaji wa maisha ya maadili yasiyokubalika umezuia njia na utafiti ya yule ambaye ni dhaifu”, mkazo katika ujuzi kamili umezuia kutokea kwa maswali, dukuduku na mahangaiko ya kuishi; na tena, mara nyingine umuhimu wa kupindukia unaolekezwa katika mapambo ya nje na mkazo mkali katika kufuata taratibu yamezaa mawazo kuwa utunzaji wa tasaufi ya kikristo haihusiani na chochote katika maisha. Wakati furaha ya kukutana na Injili na “undugu” ilikuwa ikififishwa na sura ya Kanisa lenye huzuni na lisilokaribisha.

Kardinali Stella, kadhalika ameonesha namna Baba Mtakatifu Francisko anavyo hamasisha katika kushinda woga wa kujifungia “katika majengo yanayotupatia “usalama wa uwongo” na kutokuwa katika mazoea ya kuwa Kanisa la kujitosheleza lenyewe ambalo linajifunga kukutana na ulimwengu. Kinyume chake, kwa vijana wa leo, “inabidi tuonyeshe uso wa Kristo, ili, katika mwelekeo wake na katika uzuri, vijana waweze kugundua sifa za ubinadamu mzuri, uliopatanishwa na kudhihirika kikamilifu. Kwa maana hiyo, kuna uhitaji, hasa leo, wa kuweka katika kitovu mada ya ushuhuda wa Kanisa na uhalisia wa maisha ya Kikristo. 

Mafundisho ya uzamivu na mbini za kichungaji

Katika uinjilishaji, amekumbusha Kardinali Stella, “kabla ya maneno, mafundisho ya uzamivu na mbinu za uchungaji”, ni muhimu “ushuhuda wa waamini na upatanisho wa Kanisa”. Kiukweli, Ujumbe wa kwanza wa Injili, “unawezekana pale dunia inapoona katika wakristo na katika Kanisa uwepo ulioguswa na kugeuzwa baada ya kukutana na Bwana”, yaani, uhalisia uliobadilishwa na Neno la Injili na kuimarishwa na misimamo na uchaguzi wa  maisha yanayoakisi au kuendana na imani inayo shuhudiwa. Kwa maana nyingine wakristo wenyewe na jumuia za kikristo “wanaweza kutoa ushuhuda ambao unahatarisha zile hukumu kabla na kutoaminika mbele ya imani. Kwa nia hiyo, kuna mahitaji kwamba, “ picha ya Kanisa irudi kutoa arufu nzuri ya ujana na uvumbuzi, kwa kurudia katika mtindo wa Kristo wa “ kukaa pamoja na dunia na kushinda ile misimamo ambayo inarudisha dunia kwa muda mwingine kujifungia, kutobadilika”, kuwa na uwezo zaidi wa kuongea na kufundisha kuliko “kusindikiza njia na kusikiliza wasiwasi”.

Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana mjni Vatican, tarehe 3-28 Oktoba  2018

Kadhalika akizungumzia juu ya Sinodi ya maaskofu juu ya vijana, Kardinali Stella ameonesha njia mbili pendelevu za kukutana na Kristu, kwanza : Neno la Mungu na Liturujia. Kwa hali hiyo, amesisitiza ni kwa namna gani vijana wa leo wataweza kukutana na Yesu, yaani katika “kuona uso wake, kuacha kuulizwa Naye na kumfuata kwa furaha”,  lakini ni katika kipimo ambacho “ tutawasidia kuishi uzoefu wa mahusiano haya na Yesu kwa kupitia Neno la Mungu”. Kwa upande wa liturujia, kulingana na Kardinali Stella, anathibitisha kuwa ni katika “ mazingira ambapo mara nyingi yamekuwa yakitelekezwa mno au kukazia mno muonekano wa nje kiasi cha kufanya liturujia iwe sehemu yenye mapambo na kumbe ni maskini wa kile kilichopo.

05 October 2018, 10:01