Tafuta

Malaika Mkuu Mikaeli ni mlinzi mkuu dhidi ya shetani mwovu Malaika Mkuu Mikaeli ni mlinzi mkuu dhidi ya shetani mwovu 

Padre Lombardi:Sura ya Maria na wanawake jasiri wa Biblia!

Padre Lombardi, Msimamizi wa chama cha Wanawake Vatican na ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Radio na msemaji mkuu wa Vatican, kwa sasa ni Rais wa mfuko Papa Mstaafu Benedikto wa XVI,ametoa mahubiri yake akitazama kwa karibu sura ya Mama Maria na wanawake jasiri katika Biblia

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Ninayo furaha kubwa kukaribishwa kwa mara nyingine tena kuadhimisha pamoja  nanyi katika mchakato wa hija ya chama chenu. Wakati nikiandaa mahubiri yangu, nimefikiria kujikita katika baadhi ya ushauri wa hivi karibuni wa Baba Mtakatifu, ambao ahuko mbali na hali halisi ya mvutano hasa katika umakini ndani ya Kanisa na kwa maana nyingine ni Kanisa ambalo kwa namna moja lina tuunganisha sisi wote. Lakini ni vema kwa imani na hata kwa ushiriki wa kweli, tunaweza kujikita kwa sala ya Pamoja na  Muungano wa Kanisa  kujikabidhsi katika nguvu ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya Papa katika shughuli yake ngumu”. Huo ndiyo mwanzo wa mahubiri ya Padre Lombardi, Msimamizi wa chama cha Wanawake Vatican na ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa RadioVatican na msemaji mkuu wa Vatican, kwa sasa ni Rais wa mfuko Papa Mstaafu Benedikto wa XVI, wakati wa kuadhimisha misa takatifu, kwa wanachama cha Wanawake Vatican tarehe 17 Oktoba 2018 katika Parokia ya Mtakatifu Anna mjini Vatican.

Akiendelea na mahubiri yake amesema, ni kipindi cha mwezi wa Oktoba, ambapo katika utamaduni, ni mwezi wa Mama Maria na kusali Rosari Takatifu. Papa Francisko amehimiza kufanya mazoezi  hayo, hata kutoa ushauri wa kuunganisha sala mbili, moja ikimwelekea Mama Maria na nyingine ya Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu. Kwa maana hiyo pendekezo la liturujia hii inajikita katika Misa za Mama Maria hasa ya  Maria Mama wa Kanisa. Na kama inavyoonekana katika sala mbili zilizo pendekezwa na Papa, kwa kina zinaunganisha katika maandiko ya liturujia ya masomo yaliyosoma, amebainisha Padre Lombardi. Akiendelea na ufafanuzi wa mahubiri yake amejikita kwa hakika katika  masomo kutoka katika kitabu cha Mwanzo 3, 9-15.20; Juditta, 13, 18-19; na Injili ya Yohane. 19, 25-27, na kwamba maandiko matakatifu ambayo kwa utamaduni wa kikristo unatazama sura ya Maria na kama ilivyo sikika katika masomo, hayo siyo maandishi ambayo si ya kina, na mabayo yanayoamsha hisia na uzoefu wa maisha yasiyo kuwa na mivutano na migogoro. Badala yake ni maandiko yanayohusu mapambano au  kwa maana nyingine ya mapambano ya kifo.

Akitazama kitabu cha Mwanzo, anasema kinachojulikana vema, na ambacho kinazungumzia juu ya dhambi, na matokeo yake. Nyoka aliye mdanganya mwanamke wa kwanza, mama wa wote wanaoishi, na hivyo ndiyo ikaanza historia ya mateso na matatizo. Kizazi cha Eva kitakanyagwa kichwa cha nyoka, lakini nyoka pia ataendelea kufuatilia uzao wa Eva na kutafuta namna ya kuwauma nyuma kwa ghafla yaani katika  kisigino chao wakiwa katika safari yao ndefu. Kizazi cha Eva ambacho kinakanyaga kichwa cha nyoka, kwa wakristo  tangu karne nyingi wamemwona Yesu, lakini hata kuona  Eva mpya, Mama wa Yesu ambaye daima anaoneshwa kwa tendo la kukanyaka ibilisi, shetani, na ambaye ndiye imani ya watu waamini wa Mungu katika safari, kama anavyosema Papa Francisko, kuwa ni mama yeye asiye na dhambi na daima hana dhambi tangu kuutungwa kwakwe, na tangu wakati ule wa uwepo wake. Kwa maana hiyo, tangu kurasa za kwanza za Maandishi Matakatifu, ubaya na mwanamke viko pamoja sambamba katika mapambano ya kweli, japokuwa mwanamke mpya atakuwa ishara na chombo cha wokovu na ushindi.

Wimbo wa katikati umetolewa katika Zaburi ya 150, ni wimbo mzuri wa Biblia. Ni wimbo ambao kwa  wazalendo wa Betulia, katika mji ambao ulikuwa umezingirwa  kwa nguvu ya wanajeshi waliokuwa wanaongozwa na Jenerali Oloferne wa Nabucodonoso, na ambaye alifanya  sikukuu wakati huo huo akajitokeza Judita. Huyo ni mwanamke shujaa ambaye aliokoa mji, mara baada ya kumkata kichwa Oloferne, katika hema lake wakati wa usiku mahali alipokuwa amemkaribisha kutokana na kupumbazwa na uzuri wake. Judita alichukua fursa yakumlewesha hadi akajisahau na ndipo akamkata kichwa. Judita alikuwa ni mwanamke mjane na mwenye maisha matakatifu, ambaye hakukata tamaa, mwenye akili na karama zake za kike, aliweza kuwakomboa watu wake na nguvu zilizokuwa zimewakwandamiza na jeuri na mharibifu, ambaye ukiwa mbele yake, ilikuwa kama umepotea.  Katika somo hili, linaonesha kwa dhati mwanake peke yake, lakini mwenye nguvu ambayo inawaokoa watu wengi kutokana mikononi mwa  utumwa na kifo, kwa kushida nguvu ya ubaya kwa namna hiyo ya kiajabu.

Kwa njia hiyo, wimbo wa Judita anayemshukuru Mungu, kuna sauti kubwa inayoonesha mapambano ya mwanamke dhidi ya nguvu ya ubaya, mapambano ambayo yanasaidiwa na Mungu na kuonesha ushindi mkuu. Hata hivyo pia ni wimbo ambao unasika katika kitabu  cha Waamuzi, mahali ambapo waisraeli wanamsifu Joeli, shujaa mwingine kama  Judita, ambaye  alimuua adui Jenerali Sisara, ishala ya vurugu na mahangaiko ya watu wake. Pamoja na  kusifu pia ipo sauti nyingine ya “salam ya Elizabeth kwa Bikira Maria aliyekwenda kumtembelea. Ni maneno ambayo kiutamaduni wa kikristo yamepokelewa daima katika sala ya Salam Maria  “wewe umebarikiwa kuliko wanawake wote….” . Kwenye wimbo wa Judita, na wanawake mashujaa wa Historia ya Israeli, Maria ni yule anayejitwisha uhuru kutoka katika ubaya unasonga na kuwafanya watumwa na  ambao unaua. Jidita alipambana kwa kutumia silaha ya imani na uzuri wake; Maria kwa unyenyekevu wake anapokea mapenzi ya Mugu kwa imani na umama wa Mungu. Padre Lombardi pia akufafanua zaidi, amejikita kuelezea Injili, kwamba Mama wa Yesu mara baada ya kukaa katika kivuli kirefu cha  maisha yake ya umma, sasa yupo kwa kwa hakika. Yeye anaonekana  chini ya Msalaba akiwa na uchungu, lakini kidete katika imani, anapokea fumbo ambalo ni vigumu kulitambua.

Ni fumbo ambalo linatimizwa na kuhitimishwa na mapambano ya kifo kati ya Yesu na ubaya, kati ya Yes una mfalme wa dunia hii. Maria anatazama na kushiriki fumbo hili. Alisindikizwa na wanawake waamini wa Galilea na ambao tayari tumejifunza kuwatambua, kwa namna ya pekee Maria Magdalena, kama kiongozi wao mkuu. Lakini pia uwepo wa mama unatoa jambo moja la kipekee.  Kama alivyokuwa amepokea kwa imani na katika mwili wake fumbo, wakati wa kutungwa kwa Yesu, ndivyo anapokea kwa upya fumbo la kujitoa binafsi katika kifo; anapoka kwa uchungu, lakini kwa kumkabidhi hata sasa kwa Mungu na hatima yake. Kutokana na hilo, kwa hakika anastahili kuwa mama wa wote waamini na wote ambao Yesu mwenyewe anakufa msalabani kwa ajili yao na ambao wanapkea upendo huo kwa imani. Kama ilivyokuwa kwa Eva, mama wa watu walio hai,  Mama Maria ndivyo anakuwa mama wa waamni na zaidi kwa wote waamini waliokobolewa na Yesu kwa kumwa damu kutoka katika mouo wake ulichomwa na kufunguka kwa ajili yetu.

Kama sala mbili zilizopendekezwa na Papa, ni sala za matumaini, wakati wa mapambano kati ya wema na ubaya ambao unatusikikiza katika historia yetu yote. Hali hii ya mapambano lakini isitushangaze, anabainisha Padre Lombardi. Sala hiyo inaanza na“Sub tuum praesidium”maana yake tunaukimbilia ulizni wake,  ni mantiki ya kijeshi ambayo inatafsiriwa  katika ulinzi, lakini ulinzi dhidi ya adui ambaye anashambulia na kuua. Badaye inasema juu ya majaribu na hatari ambamo tunatafuta kimbilio. Ni sala ya Maria ambayo ni ya kizamani sana na labda ndiyo ya zamani sana tuliyo nayo kwa maana inapatikana tayari katika kurasa za kwanza kwa watafiti ambao wanahesabu katika karne ya tatu na iligunduliwa huko Alexandria nchini Misri. Siyo sala ya binafsi bali ya watu wote kwani ni katika wingi, ni ya watu ambao wanahisi kushambuliwa na majaribu na hatari kubwa. Labda ilitungwa wakati wa mateso ya mwisho ya utawala wa kirumi, kipindi cha wafiadini. Sala inamtazama Maria kama Mama Mtakatifu wa Mungu na kwa maana hiyo anapewa jina kubwa ambalo baadaye litajulikana rasmi na Mtaguso wa Efeso na baadaye kuwekwa msimamizi wa Kanisa Kuu Mtakatifu Maria Mkuu Roma. Lakini hata hivyo inaonesha hata kama Bikira , ambaye katika maandiko asili, ni Bikira asiye kuwa na doa. Kutokana na ibada kuu ya upendo wa watu wanaoteseka, Papa Francisko anawalika kumwelekea Maria mlinzi, msimamizi katika roho ya mshikamano na Kanisa lote katika kipindi cha majaribu.

Sala ya Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, hiyo ni ya karibuni, ambayo, ilitungwa na Papa Leone XIII kwenye miaka1800. Kwa wale ambao ni wazee, wanatambua kuwa sala hiyo ilikuwa inajulikana sana kwa maana ilikuwa wanaisali kila misa hadi walipofanya mageuzi ya liturujia ya Mtaguso. Wakati wa kusali, walikuwa wanasali kwa haraka na wakati huo, ilikuwa inatajwa hayo majina ya shatani na jehanamu, sala hii haikupendwa sana tofauti na ile ya Tunaukimbilia ulnzi wako, ambayo mara nyingi inaimbwa katika kwa wimbo mzuri wa kilatini. Lakini kutokana na kwamba Baba Mtakatifu ameiweka sala hii ya pili ni muhimu kufanya hivyo, amethibitisha Padre Lombardi. Papa Francisko anahimiza kusali kwa sababu ya ubaya wa shetani na kutafuta kutambua ulaghai wake. Shetani anayo majina mengi, lakini ni yeye tu, kwani anitwa, joka la kizamani, mdanganyifu; ibilisi, yaani mtengenishi; shetani yaani adui na mshitaki mkuu. Papa Francisko anakumbusha juu ya maandiko matakatifu, kama Kitabu cha Mwanzo wa somo lilosikika, lakini hata katika Kitabu cha ufunuo, ambapo wanazungumza mapambano kati ya wema na ubaya, kati ya Mungu na shetani , katika kipindi chote cha histria ya dunia hii. Kwa mantiki hiyo katika kurasa hizo zinaonesha umuhimu wetu sisi kusali na hata kurudisha sura ya mwanamke.

Katika sura ya 12 ya kitabu cha ufunuoa ambapo mara nyingi tumesikia wakati wa sikukuu ya kupalizwa Maria mbinguni, wanazungumza juu ya ishara kuu inayo onekana juu mbinguni; mwanamke aliye vikwa jua na  taji la nyota 12 juu ya kichwa chake na chini ya miguu yake. Mwanamke ambaye anafukuzwa na joka kuu la kutisha likitaka kumlalua mtoto aliyezaliwa. Lakini kitabu kitakatifu kinaendela: ndipo vita kuu mbinguni inatokea: Mikaeli na malaika wake wanapigana na joka kuu. Joka kuu, la kizamani, ambaki tunaliita ibilisi na shetaia mwenyewe analaghai dunia nzima, anaangushwa chini ya ardhi akiwa pia na malaika wake. Pamoja na hayo, baada ya kuanguka kutoka mbingini hadi ardhini, joka hili linaendelea kumshambulia mwanamke.  Anashindwa kumla, lakini anaendelea na vita dhidi ya uzao wake dhidi ya wale ambao wanajaribu kufuata amri na kuwa mali ya ushuhuda wa Yesu. Kwa hakika hadi katika mwisho wa dunia hii, shetani anaendelea kuonekana na kuwadhuru watu wa Bwana. Maria ni ishara na ahadi ya wokovu, ya ushindi wa mwisho ambao tayari upo kwa neema ya damu ya Yesu na sisi tunapaswa kuutazama kwa imani kuu. Mikaeli anapigana na adui mwovu, lakini pia hata sisi tunapaswa kuendelea kujitazama kwa maana yeye anaendelea kuizunguka dunia, ili kutufanyia mabaya.

Yesu, mwanakondoo aliyechinjwa na mshindi: Padre Lombardi amehitimisha mahubiri yake akisema hiyo ndiyo hali hal isi ya kitasaufi ya Maandiko matakatifu na sala mbili ambazo Papa Francisko amependekeza na ili ziweze kutusaidia kutembea katika safari ya maisha. Historia na maisha, vinaendelea kukumbwa na mapambano kati ya wema na ubaya, kati ya Mungu na ila za Shetani ambaye ni mwenye roho mbaya. Yesu, mwanakondoo aliyechinjwa na mshindi ambaye anazungumziwa katika Kitabu cha Ufunuo, amesha tukuomboa kwa damu iliyomwagika juu ya msalaba. Maria amekuwa mama yetu akiwa msalabani, watakatifu malaika na watakatufu wote wanatusindikiza na kutusaidia: Tuishi uwepo na mshikamano wa pamoja na kutazana utakatifu wao na msaada wao. Kwa njia hiyo tunaweza kweli kutoa viini macho na kishinda kila siku maingilio ya ibilisi ambaye anajitokeza katika maisha yetu binafsi hata kijumuiya. Kwa mshikamano na sala, tuhifadhi na kuongeza umoja wa Kanisa tukiwa pamoja na Papa.

20 October 2018, 14:54