Tafuta

Balozi wa Kitume nchini Iraq na Jordan Balozi wa Kitume nchini Iraq na Jordan 

Nchi Takatifu:Mkutano wa maaskofu katika mada ya ndoa na wahamiaji!

Maandalizi ya Sakramenti ya ndoa ni muhimu ili kupunguza maombi ya kubatilishwa kwa ndoa, ambapo inazidi kuongezeka hata katika jumuiya za kikristo nchi Takatifu za Mashariki. Ndiyo ushauri unaojionesha katika Waraka wa mwisho wa Mkutano Mkuu wa Wakatoliki nchi Takatifu (Aocts) ulioanza tarehe 25-26 Septemba 2018.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mkutano huo ulifanyika huko Amman nchini Jordan, na maaskofu kutoka nchi za Jordan, Palestina, Israeli  na Cipro unathibitisha kuwa: “Maandalizi ya Sakramenti ya ndoa ni muhimu ili kupunguza maombi ya  kubatilishwa kwa ndoa, ambapo inazidi kuongezeka hata katika jumuiya za kikristo nchi Takatifu za Mashariki.   Ndiyo ushauri  mkuu unaojionesha katika Waraka wa mwisho wa Mkutano Mkuu wa Wakatoliki nchi Takatifu (Aocts) ulioanza tarehe 25-26 Septemba 2018.

Mkutano Katika waraka wao wa mwisho uliotangazwa na Upatriaki wa Yerusalem na kutolewa pia na   Shirika la habari la Sir,  wanathibitisha kwamba, umetathimini matunda ya kwanza nyaraka mbili za Papa za Motu proprio  “Mitis Iudex Dominus Jesus” ( Bwana Yesu, Hakimu mwenye huruma ambayo inarekebisha kanuni za mahakama ya Sheria ya Kanisa (CIC) kwa Makanisa na nyingine “Mitis et Misercors Iesus”msamaha na huruma ya Yesu ”, ambayo inarekebisha Kanuni za Makanisa katika uendeshaji wa kesi za kubatilisha ndoa kwa Makanisa ya Mashariki (CCEO). Kulingana na hilo pia umetolewa mwaliko kwa maaskofu wa Argentina “ kuwakaribisha wanandoa, kuwasindikiza , kufanya mang’amuzi katika hali yao na kutafuta kufungamanisha na wao katika maporokia ili waishi nao imani ya kina.

Mada ya wakimbizi wa Iraq na Siria kupokelwa nchini Jordan

Kati ya mada zilizogusiwa ni zile pia za kawada zinazowatazama wakimbizi wa Iraq na Sira waliokaribishwa nchini Jordan. Mkutano wao umepongeza uwakilishi wa Caritas nchini Jordan na kuwaomba wafadhili waendelee kusaidia masikini wanafunzi wa Iraq ambao wanasoma katika jumuiya zao. Aliye anzisha shughuli hiyo ya ukarimu ni Baraza la Maaskofu wa Italia kwa miaka mitatu ya mwisho. Kuhusu mada hiyo, hata Padre Rafic Nahra, Patriaki msaidizi wa wakatoliki kwa lugha ya kiyahudi nchini Israeli na muhusika wa maandalizi ya kichungaji kwa ajili ya wakimbizi wanaoomba hifadhi nchini Israeli, amezungumzia juu ya “ furaha na changamoto za kichungaji kwa wahamiaji, na kufafanua shauku ya kuwa na mpango wa kufanya  maandalizi ya kichungaji hata katika maeneo ya Cipro na nchini Jordan , nchi ambazo zinakaribisha maelfu ya wafanyaazi wageni.

Kuonesha hali halisi ya Kanisa nchini Jordan

Katika Mkutano huo uliuodhuriwa hata na Balozi wa Vatican nchini Jordan na Iraq Askofu Mkuu Alberto Ortega, Askofu Mkuu Leopoldo Girelli, Balozi wa Vatican nchi za Israeli na Cipro na wawakilishi wa kitume kwa ajili ya Yerusalem na Palestina, Askofu Mkuu Ortega, akiwakilisha hali halisi ya Kanisa nchini Jordan amethibitisha kuwa “ uhusiano na Serikali ni mwema na Kanisa linaonja kwa sasa uhuru wa dini” , amesisitiza pia kuwa, nafasi maalum ya mfalme katika msimamo wa kisiasa wa Ufalme wa Hashemita, licha ya ukosefu wa usalama katika mipaka ya nchi ni mzuri”

 Mahusiano ya Vatican na Serikali ya Israeli na kati ya Vatican na Serikali ya Palestina

Askofu Mkuu Girelli Balozi wa Vatican nchini Israeli na Palestina, amezungumza pia juu ya mahusiano kati ya Vatican na Serikali ya Israeli na kati ya Vatican na Serikali ya Palestina, na kwa namna ya pekee juu ya mchakato uliopo wa Israeli kuhusu hali halis ya mkataba iliyotiwa saini tayari . Hata hivyo katika salam zao za mwisho wamezitoa kwa Mababa wa Sinodi watakaoshiriki Sinodi kuhusu vijana, inayoanza tarehe 3-28 Oktoba. Na pia  mkutano wao mkuu wa maaskofu wa nchi Takatifu, unatarajiwa kufanyika mjini Tiberiade, kunako tarehe 12 na 13 Machi 2019.

Ndugu wapendwa wasikilizaji na wasomaji wa Habari zetu za Vatican News, ebu tujikumbushe juu nyaraka hizi mbili za “Motu proprio”zinazolenga  kufanya mabadiliko katika Mfumo wa Mahakama ya Kanisa Katoliki juu ya uendeshaji wa kesi zinazohusiana na sheria ya ndoa. Papa alitoa nyaraka Motu proprio, “Mitis Iudex Dominus Jesus”au Bwana Yesu, Hakimu mwenye huruma", kunako tarehe 8 Septemba 2015 ambayo inarekebisha kanuni za mahakama ya sheria ya Kanisa (CIC) kwa Makanisa ya Amerika na barua nyingine, “mitis et misericors Jesus" yaani Msamaha na huruma ya Yesu”, iliyotolewa kunako tarehe 15 Agosti 2015 ikiwa ni Sikuu ya Bikira Maria na pia mwaka wa tatu tangu Baba Mtakatifu achaguliwe kuwa Papa, ambayo  inarekebisha Kanuni za Makanisa  katika uendeshaji wa kesi za kubatilisha ndoa kwa Makanisa ya Mashariki (CCEO).

Mambo ya kuzingatia katika Marekebisho ya mchakato 

Kuhusiana na marekebisho hayo kuna mabadiliko maalum matatu , hasa katika uharakisha wa kushughulikia kesi za wanaondoa wanaotaka kubatilisha ndoa; kuondolewa kwa haja ya mahakama kutoa hukumu mara mbili kwa tukio na kisha tena kupelekwa katika mahakama ya rufaa, kwa maana kwamba, inatosha kuzingatia maamuzi yaliyotolewa na mahakama kwa mara ya kwanza, iwapo yanayoona kwamba, kuna ushahidi wa kutosha kwa ndoa kutanguliwa, na wahusika wanaweza kufunga ndoa ndoa mpya kwa mujibu wa sheria Kanisa (au katika kupokea miungano ya ndoa ilifungwa kwa sheria za kiraia , wakati huo huo kutambuliwa na Kanisa).

Pia kuanzishwa kwa uwezekano wa kesi kusikilizwa na hakimu mwenye uzoefu mara moja, kama hatua ya kupunguza mzigo wa wingi wa kesi katika mahakama za majimbo, ambako watu wenye ujuzi ni wachache); Na uundaji wa kueleka mchakato wa kesi katika baadhi ya kesi, kutolewa maamuzi moja kwa moja na Askofu mahalia, kwa kesi ambazo zina ushahidi wa kutosha kutolewa hukumu ya kubatishwa na pande zote mbili zinaamini muungano wao ulikuwa batili. Katika mchakato huu hasa unaonyesha dhamira Papa Francisco kugawana madaraka na Maaskofu wa majimbo duniani kote.

Uvumi wa baadhi ya vyombo vya habari 

Pamoja na hayo  kinyume na uvumi uliotolewa na baadhi ya vyombo vya habari za kijamii na hata katika vyombo vya Kanisa, mabadiliko yamefanyika katika misingi ya uelewa wa Kanisa la asili na muundo wa kimsingi wa ndoa, na hivyo hakuna mabadiliko katikaMadhumuni msingi na katika wigo wa mfumo wa Mahakama wa Kanisa. Na wala hakuna mabadiliko katika mafundisho ya Kanisa juu ya kutengua ndoa, na kwa maana hiyo, nyaraka mpya za mabadiliko hazibadilishi kanuni zinazofuatwa na Mahakimu katika kubatilisha ndoa na wala hazibadili uhalali wa ndoa, hivyo, ndoa kubatilishwa linabaki ni jambo linalohitaji uwepo wa ushahidi wa kutosha.

Na hili ni suala ambalo tutazidi kila mara kurudia kutokana na kwamba watu wengi, hasa zaidi vyombo vya habari, na mitandao ya kijamii, wasio soma kwa makini na kuwa na uelewa, wanazidi zaidi kuendeleza uongo zaidi na kuvumisha kile ambacho hawajaelewa vizuri juu ya kanuni hiyo na nyaraka hizi mbili za Baba Mtakatifu; kwa maana hiyo ni lazima kuzifahamu vizuri, bila kuchanganya watu wengi.

 

01 October 2018, 10:21