Vatican News
Tarehe 14 Oktoba anatangazwa Mtakatifu Papa Paulo VI Tarehe 14 Oktoba anatangazwa Mtakatifu Papa Paulo VI  (Vatican Media)

Mahujaji elfu 5 kutoka Brescia na Concesio kwa ajili ya Paulo VI

Jumuiya kutoka Brescia nchini Italia, wanajiandaa kufika katika Siku ya kumtangaza Mwenyeheri Papa Paulo VI kuwa Mtakatifu. Watakuwa ni maelfu ya mahujaji watakaofika mjini Vatican kwa ajili ya maadhimisho yanayotarajiwa tarehe 14 Oktoba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu wa PierantonioTremolada wa Jimbo la Brescia, pia Paroko wa Kanisa la Concesio mahali alipozaliwa Papa Paulo VI, wanasema watu wengi wanayo shauku kubwa kufika katika maadhimisho ya kutangazwa Mtakatifu, Papa Paulo VI na kwa maana hiyo wametoa taarifa kuwa mahujai kutoka Brescia na Concesio watakuwa ni elfu tano na zaidi ya mahujaji mia sita kutoka katika Parokia ya Concesio.

Katika tovuti ya WebDOc iliyoanzishwa kwa namna ya pekee kwa ajili ya tukio hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa ya kutangazwa kwa Papa Paulo VI kuwa mtakatifu na wengine, akiwemo hata Askofu Romero, pia jambo la Brescia nchini Italia linaoesha hiyo ari na moyo wa waamini ambao watafika katika misa , ili kuonesha ukaribu wa mtu/ watu ambao walipendwa na ambao bado wanapendwa.

Naye Askofu wa Brescia Pieranotonio Tremolad amethibitisha kuwa, ni zaidi ya watu elfu tano ambao wamejiandikisha kufanya hija ya kuudhuria maadhimisho hayo. Na kwa mujibu wa taarifa kutoka parokia ya Concesio mahali ambapo, tarehe 26 Septemba 1897 alizaliwa Papa Montini, zaidi ya watu 600 wako tayari kusafiri kuja Roma, kwa njia mabasi makubwa, treni na magari binafsi.

Hata hivyo katika parokia alikozaliwa, waamini wengine wote watashiriki moja kwa moja Misa Kuu wakiwa katika uwanja wa Parokia yao wakufuatia kwenye televisheni moja kwa moja katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Na  Parokia hiyo, watu wengi wamekuwa na ibada  kuu kuelekea katika Kanisa hilo kwa ajili a kuona mahali na  kutazama , kisima cha ubatizo ndani ya Kanisa dogo kuu la kirumi liitwalo Mtakatifu Antonino Shahidi.

.

04 October 2018, 12:51