Tafuta

Askofo Mkuu Cornelius Fontem wa jimbo la  Bamenda amethibitisha kifo cha kijana mseminari Gérard nchini Cameroon Askofo Mkuu Cornelius Fontem wa jimbo la Bamenda amethibitisha kifo cha kijana mseminari Gérard nchini Cameroon 

Kifo cha mseminari huko Yaounde, Camerun

Kijana mseminari Gérard Anjiangwe, mwenye umri wa miaka 19 ameuwawa na kikundi cha wanajeshi, tarehe 4 Oktoba 2018, mbele ya Parokia katoliki ya Mtakatifu Theresa wa Bamessing, kaskazini Magharibi ya Camerun. Na Padre Gigi Maccalli kutoka Italia mmisionari nchini Niger ametekwa nyara mwezi mmoja uliopita

Sr Angela Rwezaula –Vatican

Taarifa kutoka vyombo habari za kimisionari katoliki Fides, vinasema kuwa, ameuwawa kijana mseminari mmoja katika kanda ya Kingereza mjini Yaounde nchini Camerun. Kwa mujibu wa taarifa zilizotiwa saini na askofu Mkuu Cornelius Fontem wa jimbo la Bamenda, kijana alikuwa anaitwa Gérard Anjiangwe, mwenye umri wa miaka 19 ambaye ameuwawa na kikundi cha wanajeshi, tarehe 4 Oktoba 2018, mbele ya Parokia katoliki ya Mtakatifu Theresa wa Bamessing, katika kijiji cha Ndop kata ya Ngo-Ketunjia, kaskazini Magharibi ya Camerun

Msemari Gérard Anjiangwe

Taarifa kutoka jimbo Kuu linaathibitisha juu ya tukio hilo kuwa, ilikuwa mida ya saa 9.30 asubuhi, baada ya misa, wakati mseminari Gérard Anjiangwe na waamini walikuwa nje ya Kanisa, na likafika gari moja la kijeshi likitokea barabara ya Ndop, na lilisimama mwanzoni mwa njia inayoelekea katika Kanisa. Baadhi ya maaskari walishuka katikati na kuanza kufyatua risasi.

Wakati watu wakikimbia ndani ya sakresitia na kufunga mlango, mseminari, alipiga magoti na kuanza kusali rosari.  Na wanajeshi baada ya kutaka kufungua mlango kwa nguvu na kushindwa, walimkaribia Gerardi kwa kumlazimisha aamke na kuanza kuumuliza maswali, baadaye kumwambia apige magoti na mkufyatua risasi mara tatu shingoni, akafa pale pale. Katika taarifa yake Askofu Mkuu Cornelius Fontem, anatoa wito kwa wakristo wote katika kipindi hiki cha uchungu, kusali kwa ajili ya roho ya Gérard na kwa ajili ya wazazi wake Stephen Akiata na Comfort Akiata, kwa maana mseminari huyo alikuwa ni mwana. 

Na huko nchini Niger, Padre Gigi Maccalli ametekwa nyara

Ni muhimu kwetu sisi katika mji wa Crema, katika Baraza hili la tarafa, ambayo inajieleza ukaribu wetu kwa familia ya Padre Gigi Maccalli,na watu wote wa Madignano wanataka kumkubatia ndugu yao wakati, na wakati wakituma ujumbe huu kupitia  Wizara ya mambo ya nchi za  nje. Katika ujumbe huu ni kuta kuonesha  umakini mkubwa kwa ajili ya kesi ambayo umegusa kwa kina jumuiya yetu na wasiwsi ambao umejitokeza kwa familia yake na mtoto huyo mkaribu”. Ni ujumbe uliotoka wa Baraza la Wilaya ya Crema nchini Italia mahali anapozaliwa mmisionari Padre Luigi Maccalli aliyetekwa nyara huko  Niger mwezi mmoja uliopita.

Hakuna habari yoyote tangu tarehe 17 Septemba, lakini hii ni kimya ambayo katika kesi kama hiyo, wanaitumia vyombo vikuu vya upelelezi kama (Farnesina Italia na Vatican) ambao wanaheshimu kwa kufikiria mafanikio, ambayo yametokea nyakati zilizopita kwa kesi kama hii. Pamoja na hayo, habari tangu tarehe 17 Septemba zilizotolewa na Shirika la habari za Kimisionari Fides linasema, kikundi cha watu wasio julikana walishambulia kituo cha kimisionari cha Bomoana huko Niger na kuondoka na Padre Pierluigi Maccalli, padre mmisionari kutoka Crema Italia, ambaye  kwa miaka mingi anakijikita katika shughuli za kimisionari barani Afrika.

Na tangu wakati huo hadi sasa hakuna sasisho lolote kutoka nchini Niger. Na hata kupata utambulisho wa wale waliomteka nyara, labda ni majihad kutoka karibu na nchi ya Burkina Faso; wakati huo huo hawajuhi hata lengo na hata kupata kujua  hali halisi ya Padre Maccalli. Katika Barua ya watu wa Crema wanaonesha wasiwasi mkubwa na huzuni, uliopo katika familia ya Padre Maccalli na watu wote ambao kwa sasa wanaishi katika kimya kikubwa, na ambacho kimetukia mbali kijiografia lakini wakiwa kwa hakika wako karibu sana katika jumuiya yao kiroho na kusali kwa ajili yake apatikane.

 

17 October 2018, 14:23