Tafuta

Vatican News
Kardinali Nzapalainga Askofu Mkuu wa Bangui, Afrika ya Kati Kardinali Nzapalainga Askofu Mkuu wa Bangui, Afrika ya Kati 

Kard.Nzapalainga ashutumu wageni wanaozuia kuishi udugu!

Kardinali Nzapalainga amewahimiza waumini kuishi kauli mbiu iliochaguliwa na Jimbo Kuu hilo isemayo:“Wakristo wa Jimbo Kuu la Bangui, katika Jina la Kristo tunazungumza na ndugu. Kardinali ameshutumu uwepo,wa wafanya biashara wageni walioalikwa na baadhi ya ndugu zao kwa sababu za kisiasa, kiuchumi, kikabila, na kibinafsi na kuzuia kuishi kidugu

Baada ya miaka 125 ya Uinjilishaji, Jimbo kuu la Bangui, sasa limetuma mapadre katika utume wa umisionari. “Ni ishara ya uhai wa makanisa yetu mahalia na ushirikiano kati ya makanisa”. Hayo yamesema na  Kardinali Dieudonnè Nzapalainga, Askofu mkuu wa Bangui, katika mahubiri yake katika Misa Takatifu ya ufunguzi wa mwaka wa Uchungaji Jumapili, tarehe 30 Septemba 2018 katika Kanisa Kuu lililopo mji mkuu wa Afrika ya Kati.

Kardinali amewahimiza waumini kuishi kauli mbiu iliochaguliwa na Jimbo Kuu hilo isemayo: “Wakrito wa Jimbo Kuu la Bangui, katika Jina la Kristo tunazungumza na ndugu zetu”. Katika mahubiri hayo, Kardinali ameshutumu uwepo, ndani ya nchi na kusema: ambayo ni nyumba ya pamoja, wafanya biashara wageni walioalikwa na baadhi ya ndugu zetu kwa sababu za kisiasa, kiuchumi, kikabila, na kibinafsi”.

Kardinali amesisitiza na kusema kuwa, wafanyabiashara hawa wageni, “wana lengo la kukaa pamoja na kufanya mazungumzo kuwa magumu nchini”. Mpaka sasa makundi yenye silaha za moto na wale wanaowawezesha kwa tamaa ya mali zilizopo katika nchi yetu”. “Kutajirika kwa kasi na kupindukia kwa baadhi ya wenzetu kwa njia ya kuharibu wengine kunatupa wasiwasi sana”, amesema Kardinali.

Kardinali amehitimisha kwa kusema: “Bwana atuepushe na ubaguzi, chuki, hasira mbaya, na kulipiza kisasi. Bwana atutie katika mioyo yetu uaminifu, uvumilivu na wema. Bikira, Mama wa wabangi, na  Malkia wa amani, atufundishe kuzungumza na ndugu zetu katika upendo na kweli”.

08 October 2018, 10:50