Vatican News
Matatizo ya ajira nchini Afria ya kusini ndiyo yanakabiliwa  uso  kwa uso kwa wanawake na vijana Matatizo ya ajira nchini Afria ya kusini ndiyo yanakabiliwa uso kwa uso kwa wanawake na vijana 

A.Kusini:Lazima kuhusisha wanawake na vijana zaidi katika kazi!

Utafanyika mkutano kuhusu kazi mwaka 2019 nchini Afrika ya Kusini, na kwa maana hiyo Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini wanakaribisha mkutano huo uwahusishe wanawake na vijana zaidi katika ustawi bora wa nchi yao

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Matatizo ya ajira nchini Afrika ya kusini ndiyo yanakabiliwa  uso  kwa uso na vijana, na kwa maana hiyo, “Tunayo matarajio makubwa kutoka kwa wanawake  vijana wasio kuwa na ajira kuwa wawakilishi wazuri katika mpango mzima unatafuta namna ya suala hili la kipeo cha ajira. Na hatuwezi kuzungumza juu yao bila kuwa nao. Ni vema kuwahusisha wanawake na vijana zaidi”. Haya yamethibitishwa na Askofu Abel Gabuza, Askofu wa Jimbo la Kimberly na Rais wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini. Ni katika ujumbe wake alioutoa kwa rais,  Bwana  Cyril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini  ili  kuhakikisha kunakuwepo mchanganyiko wa uwakilishi wa kazi kwa upande wa wanawake na vijana katika Jukwaa kuhusu kazi, Jukwaa linalitarajiwa kufanyika mwaka kesho 2019.

Pongezi ya kupyaisha mipango mipya

Licha ya maombi hayo pia Askofu Gabuza ameonesha furaha yake, “ kwa ajili ya uongozi wake rais hasa  kuhusiana na  chachu ya sasa ya kutaka kupyaisha mipango, pamoja na maamuzi yake ya kuimarisha mipango mipya ya uwekezaji. Askofu Gabuza anamwalika Rais kupitia  chama  chake tawala ambacho kinaonesha hatima ya maendeleo ya taifa ambayo bado hayajawa ya kweli, kwa maana hiyo ni mtarajio yao wanaweza, “kuongoza  vema katika matokeo ya usimamizi unao hitaji kutekelezwa katika hali halisi ya uchumi.

Idadi ya watu wa Afrika Kusini inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi, kuongezeka kwa bei ya vitu vya msingi, na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira. Mashirika mengine ya kiraia yameomba  hata ruzuku ya kipato cha msingi na kutazama kwa upya  juu ya misaada wa mshahara kwa vijana. Amehitimisha Askofu Gabuza akisema: “Tunatarajia kuwa rais na baraza lake la mawaziri watatafakari kwa makini mapendekezo hayo”.

Matarajio ya serikali kuongeza idadi ya watu walio ajiriwa, kutoka kwa milioni 11 hadi milioni 24

Mkutano wa mwaka huu wa kazi ulifanyika tarehe 4 na 5 Oktoba 2018. Kulingana na Rais Ramaphosa, mipango na makubaliano ya ajira wamekubaliana na washiriki kuundwa kwa ajira 275,000 kwa mwaka. Takwimu juu ya ajira nchini Afrika Kusini zinaoneesha kuwa, pamoja na ukuaji wa  ajira ya nafasi  206,000 katika robo ya pili ya 2018, lakini bado kuna  kiwango cha ukosefu wa ajira wenye  27.2%.   Kwa mujibu wa mpango wa kitaifa wa maendeleo, serikali inatarajia kuongeza idadi ya watu walioajiriwa, kutoka kwa milioni 11 hadi milioni 24 kufikia mwaka 2030.

16 October 2018, 13:56