Kupinduka kwa feri nchini TANZANIA  Kupinduka kwa feri nchini TANZANIA  

Tazania:Uchungu wa Papa kwa waathirika wa ajali ya meli!

Papa Francisko anaelezea masikitiko yake mara baada ya kupata habari ya ajali ya feri ya MV Nyerere ambayo ilipinduka katika Ziwa Victoria,ufukweni mwa Kisiwa cha Ikara tarehe 20 Septemba 2018. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tazania ametangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa kuanzia Ijumaa 21 Septemba

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake, uliotiwa saini na Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican tarehe 21 Septemba 2018 kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania Askofu Marek Solczynsk, kufuatia na Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa raia, viongozi wa Kanisa, na  Serikali ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kufuatia ajali ya meli iliyotokea, Alhamis 20 Septemba Tanzania.

Masikitiko ya Papa Francisko kwa waathirika

Baba Mtakatifu Francisko anaelezea masikitiko yake mara baada ya kupata habari ya ajali ya feri ya MV Nyerere ambayo ilipinduka katika Ziwa Victoria, ufukweni mwa Kisiwa cha Ikara tarehe 20 Septemba 2018. Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anaonesha kwa masikito moyoni na  mshikamano kwa wale wote wanao omboleza kwa ajili ya kupoteza wapendwa wao na kwa wale ambao bado wanahofia kuwakuta bado hai wale ambao hawajapatikana. Kwa wote anaomba baraka ya Mungu iwashukie na kuwakumbatia kwa nguvu na faraja kwa wale waliopatwa na mkasa huo. Kadhalika anawatia moyo viongozi wa raia na vikosi vya ukoaji wanaoendelea katika juhudi hiyo ya uokoaji.

Habari ya tukio la MV Nyerere kuhusu  kuzama kwa kivuko wilaya ya Ukerewe, Mwanza, Tanzania. Kivuko kilichopewa jina MV Nyerere kilizama Alhamisi adhuhuri kikitokea bandari ya Bugolora katika kisiwa cha Ukerewe kuelekea katika kisiwa cha Ukara. Rais wa Jamhuri ya  Tanzania Bwana John Magufuli amesema watu 131 wamethibitishwa kufariki kufikia sasa na watu waliookolewa ni 40, huku shughuli za uokoaji zikiendelea. Ameagiza kuundwa kwa tume ya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo na kusema kuwa wote waliochangia kusababisha ajali hiyo watachukuliwa hatua kali.

Rais pia ametangaza siku nne za maombolezo ya kitaifa kuanzia Ijumaa 21 Septemba ambapo pia ameamrisha kuwa bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti kwa siku tatu kuanzia Jumamosi. Idadi rasmi ya waliothibitishwa kufariki ni 131, kwa mujibu wa tangazo la Raisambaye alihutubiwa taifa kwa kupitia runinga siku ya Ijumaa jioni 21 Septemba. Baadaye taarifa kutoka ikulu ilitolewa ikithibitisha idadi hiyo.

 

22 September 2018, 10:01