Tafuta

Vatican News
Migogoro ya kivita huko Idlib nchini Siria bado inaendelea na watu wako hatarini Migogoro ya kivita huko Idlib nchini Siria bado inaendelea na watu wako hatarini  (AFP or licensors)

Siria:Ipo hatari ya mji wa Idlib kuendelea na mauaji kwa raia!

Sista Youla Girges, mtawa mfransiskani wa wamisionari wa Moyo Safi wa Maria, na mzaliwa wa kijiji cha Kikristo cha Gassanieh, ambacho kwa sasa kinadhibitiwa na waasi wa Kiislamu kwa miaka saba, anathibitisha kwamba Papa ana ubinadamu wa watu wote wa Siria moyoni mwake, akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na suala la migogoro huko Idlib

 Frt Titus Kimari - Vatican

Katika mahojiano hayo Sisita anasema  Rais wa Marekani Trump hivi karibuni katika mtandao wake wa twitter, ametoa onyo kwa utawala wa Assad na kumtaka kutosababisha maafa mapya kwa binadamu Syria. Lakini  Rais Bashar al-Assad hapaswi kushambulia jimbo la Idlib nchini Syria, na Warusi na Iran watafanya makosa makubwa ya kibinadamu katika kushiriki kwenye  majanga haya makubwa ya kibinadamu, mamia ya maelfu ya watu wanaweza kuuawa.

Ripoti juu ya matumizi ya kichochezi  cha silaha za kemikali:  Sista huyo katika mahijiano anasema kuwa “hatuwezi kuruhusu hilo litokee"! Urusi kwa upande wake imetoa wito kwa shirika kuzuia silaha za kemikali bila kupuuza ripoti juu ya matumizi ya 'kichochezi' ya silaha za kemikali huko Idlib. Maendeleo Siria na kanda na pia masuala ambayo yatajadiliwa katika mkutano wa wa Urusi-Uturuki na Irani utakaofanyika mapamema Ijumaa 7 Septemba 2018 huko Tehran, ni mada ya katika mazungumzo baina ya rais wa Syria, Bashar al-Assad na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif. Assad na Zarif wamethibitisha kwamba, shinikizo lililofanywa na baadhi ya nchi za Magharibi juu ya Syria na Iran haliwezi kuwazuia kutetea misimamo yao, maslahi ya watu wao, usalama na utulivu wa kanda nzima.

Wito wa Papa Francisko kwa ajili ya Siria: Katika wito wa  Baba Mtakatifu Francisko Jumapili 2 Septemba  2018 wakati wa sala ya malaika wa Bwana,  mjini Vatican kuhusu  hali ya Idlib, Papa hakuacha kuomba kwa ajili ya watu wa Siria. Kwa maana hiyo  Sista Youla Girges, mtawa mfransiskani  wa wamisionari wa Moyo Safi wa Maria, na mzaliwa wa kijiji cha Kikristo cha Gassanieh, ambacho kwa sasa kinadhibitiwa na waasi wa Kiislamu kwa miaka saba, anathibitisha  kwamba Papa ana ubinadamu wa watu wote wa Siria moyoni. Kadhalika anaongeza kusema “Tunajua kwamba jumuiya nyingi za Kikristo bado zipo Idlib. Tuna hofu kwamba kama ilivyo katika maeneo mengine mauaji yanafanyika ... Rai ya kwanza ya Papa ni kuhakikisha kwamba raia wote wana haki maisha, ambao wamekuwa katika mikono ya waasi katili kwa miaka saba. Kutokana na wito wa Papa kwa dhati  ni ombi chanya kwa jumuiya nzima ya kimataifa ili kukuza amani na mazungumzo ya kisiasa bila vurugu, bila watu wengine kupoteza maisha.

Kijiji cha Gassanieh:  Sista Youla aanaeòeza kuwa “Kijiji changu cha Gassanieh kilidhibitiwa na waasi wa kiislamu miaka mitano iliyopita”, na  kwamba kwa sasa hawajui mwisho wake ni nini. Kuna  vijiji vingine jirani  vya kikristu ambavyo mpaka sasa kuna jumuiya za kikristu pamoja na mapadre wafransiskani. Huko wanaishi chini ya mamlaka ya waasi, wanafuata sheria zao mathalani za kiislamu.  Kadhalika anafafanua kuwa kwa mfano, katika kijijini chake cha Gassanieh, hakuna wakristu wengi maana walikimbia baada ya mauaji ya Padre François Mourad. Alipouawa, watu wachache waliokuwepo walikimbia kwa sababu maisha yao yalikua hatarini. Baada ya miaka saba ya vita, “watu wa Siria wamechoka kwasababu hawaelewi hivi vita vina maana gani hasa” na kwa maana hiyo wanaendela kuomba amani!

Wanaiomba jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kwa maslahi mapana ya watu wa Siria.H: ata hivyo anathitisha kwamba, wakristu walikuwa wanaishi vizuri sana kabla ya vita hivi. Leo hii sio, wanalazimika kuziishi sheria za ajabu, sheria inayokataza kuwa na mali, uhuru wa kujieleza, kuabudu na hata kufanya sherehe, vyote ambavyo watu walifurahia kwa amani na uhuru sasa hayawezekani. Kuhusu uwezekano wa kujijenga upya, sista Youla, anakiri kwamba inawezekana. Maridhiano na msamaha baina ya watu wote wa Siria yanaweza kufungua mlango wa mwanzo mpya. Anakumbushia kwamba vita ya Siria sio vita dhidi ya ukristo ila ni dhidi ya Siria. Waathirika ni wakristu, Waislamu, Wadrusi, Waismaeliti pamoja na makabila yote. “Tunajua kwamba Siria ilikua maarufu kwa uzuri wa makumbusho yake na amani itakaporejea tutaanza tena kujirudi na kuishi pamoja.

Huko Damasko, katika miaka miwili iliyopita tumefanya mradi wa msaada wa kisaikolojia kwa watoto walioathiriwa na vita ambapo watoto wa Kikristo na Waislamu wanakutana pamoja ili kupokea msaada huo. Kwa maana hiyo anafikiri kwamba misukosuko iliyobaki itakuwa sababu ya kuzaliwa upya, ya kuimarisha Ukristo ambao haujawahi kushindwa.

 

06 September 2018, 08:52