Tafuta

Mahojiano na Askofu Mkuu Lorefice wa jimbo Kuu la Palermo kuhusu ziara ya Papa Mahojiano na Askofu Mkuu Lorefice wa jimbo Kuu la Palermo kuhusu ziara ya Papa 

Papa akutana na Askofu Mkuu wa Palermo siku saba kabla ya ziara!

Katika mazungumzo ya Askofu Mkuu Lorefice wa Jimbo Kuu la Palermo na mwandishi wa habari wa Vatican News amesema kuwa, Papa Francisko, daima amekuwa na matarajio ya matumaini na nguvu katika Kanisa la Palermo. Ziara yake katika uwanja wa Armerina na Palermo kwa sasa unatoa mwamko mkubwa kwa waamini wote Sicilia

Sr. Angela Rwezaula  - Vatican

Tarehe 7 Septemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Askofu mkuu Corrado Lorefice wa Jimbo Kuu la Palermo wiki moja kabla ya zira yake ya kutume kisiwani Sicilia. Hii itakuwa ni miaka 8 tangu hata Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alipotembelea huko. Ziara ya Papa Francisko, inatarajiwa kufanyika tarehe 15 Septemba il kutembelea mji mkuu wa Kisiwa cha Sicilia.

Katika mazungumzo ya Askofu Mkuu Lorefice wa Jimbo Kuu la Palermo, na mwandishi wa habari wa Vatican News amesema kuwa, Papa Francisko, daima amekuwa na matarajio ya matumaini na nguvu. Ziara yake katika uwanja wa Amerina na Palermo kwa sasa unatoa mwamko mkubwa kwa waamini wote Sicilia.

Ni Kanisa ndani ya dunia lenye kuhitaji wakristo hodari

Akiendelea na maelezo yake anasema, Papa anataka kuwahimiza katika mtazamo wenye wazo la uhoadari, na hasa katika upatanisho wa Kanisa ambalo kwa uhakika linatambua kwa dhati kukaa ndani ya ulimwengu kwa shauku na furaha ya Injili. Kwa maana hiyo anataka kuwatia moyo ili hata Kanisa la Sicilia liweze kuwa Kanisa linalo nuia furaha ya kutangazwa kwa umisionari wa Injili kwa sababu, upendo wa Mungu uwafikie watu wote. Kadhalika Baba Mtakatifu anataka kuwakumbusha kuwa wote tu ndugu, na kuwaelekeza maisha ya mshikamano, wa haki na ushirikishwaji ambapo dunia leo hii inawahitaji wakristo hodari katika kushuhudia.

Padre Puglisi alitangaza Injili bila kuogopa kumwaga damu

Tarehe 15 Septamba ijayo ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu kifo cha Padre Pino Puglisi , aliyeuwawa mbele ya nyumba yake kwa mikono ya  kikundi cha uhalifu wa kupangwa kiitwacho  Mafia kwa sababu ya juhudi zake alizokuwa anajikita kwa watoto na wanye kuhitaji katika mtaa wa Brancaccio huko Palermo.

Kwa maana hiyo Askofu Mkuu Lorefice  anaongeza kusema “ Ninapendelea kumshukuru Baba Mtakatifu, kwa kuchagua tarehe hiyo na zaidi kwa ajili ya kufika kama mhujaji kwenye kaburi ya mfiadini”.  Hili ni wazo kwamba  Papa Francisko anataka Kanisa lenye uwezo wa kushuhudia , kwa ile tabasamu ya kawaida aliyokuwa nayo Padre Pino Puglisi , anataka Kanisa lenye uwezo  wa kutangaza Injili bila hofu ya kumwaga damu.

08 September 2018, 09:07