Tafuta

Vatican News
Mazungumzo na majadiliano, ndiyo nguzo ya kuleta maelewano na kushinda migogoro ya Nicaragua Mazungumzo na majadiliano, ndiyo nguzo ya kuleta maelewano na kushinda migogoro ya Nicaragua 

Njia ya mazungumzo ndiyo suluhisho la mgogoro nchini Nicaragua

Katika mkutano na waandishi wa habari Askofu mkuu na Kardinali wa Managua, Leopoldo Brenes, alitaja maandamano ambayo yanaendelea kufanyika nchini ili kupinga mgogoro wa kijamii na kisiasa unahitaji bado mazungumzo ya kweli ya pamoja ili kuweza kupta suluhisho la kweli nchini Nicaragua

Frt. Titus Kimario - Vatican

Kardinali Brenes akizungumza na waandishi wa habari  amewatakia mema  watu wa Nicaragua, kwamba wanaweza kukua, kama wanaume na wanawake, kwa kuheshimiana. Na kwa upande wa mgogoro,  alisema njia pekee ni majadiliano, kama Papa Francisko anavyopendelea kuhamasisha

Katika mkutano na waandishi wa habari Askofu mkuu na Kardinali wa Managua, Leopoldo Brenes, alitaja maandamano ambayo yanaendelea kufanyika nchini ili kupinga mgogoro wa kijamii na kisiasa unahitaji bado mazungumzo ya kweli ya pamoja. Kardinali alikumbuka maneno ya mtangulizi wake, kardinali Obando Bravo, akisema  kwamba "wakati mwingine maneno mengi yanatoka kinywani mwetu, hata kama yana vikwazo viwili: meno na midomo, lakini wakati mwingine, kama kardinali alivyosema, maneno hayo yanayotoka moyoni ni nguvu, ni mabomu, kuharibu vikwazo hivyo viwili ".

Alizungumza hayo  tarehe 2 Septemba, Kardinali Brenes alisema kuwa Yesu katika Injili anatualika kutakasa mioyo yetu, kwa sababu mambo mengi mabaya hutoka moyoni, lakini pia mambo mazuri. Ni muhimu, aliongeza kusema, kufanya kazi ili kuutakasa na kuuponya moyo wetu, Kuna kidonge kinachoponya moyo na hiki ni Injili.

Njia ya mazungumzo ndiyo suluhisho la mgogoro nchini Nicaragua: Akijibu swali juu ya kufukuzwa kwa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Askofu Mkuu wa Mangua alisema kuwa ni ya kusikitisha, kwa sababu wakati mwaliko ulifanyika kwa taasisi hizi, ilidhaniwa kuwa unapaswa kusaidia upatanisho na mazungumzo. "Kwangu binafsi, alisema, inasikitisha, lakini kama vile tunavyoheshimu maamuzi ya serikali tuna amini haitaleta matokeo ya kuwaliza watu.

Habari njema: Habari njema ni kwamba hawa wajumbe hawahitaji tena kubaki nchini, leo wanaweza kujua kuhusu hali halisi ya nchi yetu kwa njia nyingine" alisema. Ujumbe wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu ulitoka Nicaragua Jumamosi tarehe 1 Septemba, kufuatia uamuzi wa serikali ya Ortega, ambayo haikubali ripoti ngumu iliyotolewa na Tume ya hali ya haki za binadamu nchini. Hati hiyo inaonyesha serikali ya Nicaragua kama sababu kuu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Kabla ya kuondoka, ujumbe ulioongozwa na Guillermo Fernández Maldonado wa Perù, uliacha ujumbe wa shukrani, ambao ni kielelezo cha msaada uliopokelewa  huko Nicaragua, wakati wa kazi zake kati ya Juni na Agosti. Pia alielezea kwamba ataendelea "kufuatilia hali ilivyo na waathirika katika kutafuta haki yao na ukweli katika ofisi ya kikanda ya Panama".

Kardinali Brenes amewatakia mema  watu wa Nicaragua, kwamba wanaweza kukua, kama wanaume na wanawake, kwa kuheshimiana. Na kwa upande wa mgogoro,  alisema njia pekee ni majadiliano, kama Papa Francisko anavyopendelea kuhamasisha. Kardinali pia alisema kuwa, baada ya majadiliano yote, kila kutofautiana kunapotokea,  haipaswi kubaki na hasira, lakini kuna wakati ambapo mtu lazima awe chini ili kuzungumza.

08 September 2018, 08:54