Vatican News
Watu wa nchini Nicaragua wanataka amani ya kudumu Watu wa nchini Nicaragua wanataka amani ya kudumu  (AFP or licensors)

Nicaragua:Ujumbe wa Papa akiwaombea amani na mapatano kindugu

Katika ujumbe wa papa kwa Rais wa Baraza la Maakofu wa Nicaragua, kwenye fursa ya Siku ya Kitaifa itakayo fanyika tarehe 15 Septemba, Papa Francisko anasali sala kwa ajili ya watoto wapendwa wa nchi na ili iweze kuwa na amani ya kuishi kindugu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika ujumbe kwa Rais wa Baraza la Maakofu wa Nicaragua, kwenye fursa ya Siku ya Kitaifa itakayofanyika tarehe 15 Septemba, Papa Francisko anasali sala kwa ajili ya watoto wapendwa wa nchi na uli iweze kuwa na amani ya kuoshi kindugu. Askofu Mkuu wa Managua, Kardinali Brenes, amesema jinsi gani maaskofu wako hima katika kusamba mazungumzo kwa ajili ya amani.

Yesu ni mfalme wa amani, awajalie zawadi ya undugu  katika mapatano, amani na mshikamano wa kuishi kwa pamoja. Ndiyo ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko aliomtumia Rais wa Baraza la Maaskofu wa Nicaragua  Daniel Ortega, kutokana na fursa ya Sikukuu ya Kutaifa katika nchi hiyo ya Amerika ya Kusini inayotarajia kuadhimisha tarehe 15 Septemba 2018. Ujumbe huo wa tarehe 31 Agosti 2018 alioutuma, Papa Francisko anatoa pia salam za kirafiki na kuwahakikishia sala zake watoto wapendwa wa Taifa.

Kipeo cha siasa kijamii

Jumamosi tareha 15 Septemba ni maadhimisho ya miaka 197 ya uhuru mahali ambao maadhimisho yanakutana na kipeo kikubwa cha kisiasa jamii , ambacho kwa miezi kadhaa kuanzia Aprili, Nicaragua imekuwa na myumbo mkali. Kwa mujibu wa Shirika la haki za binadamu za umoja wa mataifa, wanakadiria kuwa waathirika 400 hadi sasa wakati huu kwa upande wa serikali huko Managua wao wanasema watu waliokufa ni 198.

Nafasi ya Kanisa:

Katika Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 3 Juni 2018, Papa Francisko aliungana na maaskofu mahalia, na kuonesha chungu mkubwa  kutokana na vurugu na ghasia ambazo zilisababisha vifo na majeruhi wengi , waliosababishwa na vikundi vyenye silaha wakidhibiti maandamano ya kijamii. Alikuwa amesali ili kuweza kusitisha kila aina ya umwagaji damu. Hata  Baraza la Maaskofu Katoliki wa Nicaragua,( Cen) miezi iliyopita walitoa pendekezo kama wawakili wa mazungumzo ya kitaifa kati ya raia na wawakilishi wa vyama vya kijamii na pia serikali. Waliomba  Rais Ortega kuharakisha uchaguzi mwezi machi 2019  badala ya mwaka   2021 , kwa lengo la kuweza kupambana na kushinda kipeo cha kitaifa, lakini mapendekezo hayo rais aliyakataa.

Kardi . Brenes: kusaidia mazungumnzo yasambae kwa watu

Askofu Mkuu wa Mangaua na Rais wa Cen Kardinali Leopold Brenes katika siku za mwisho amesisitiza juu ya maaskofu kuwa na mwamko wa kuweza kuendeleza mazungumzo. Kardinali anabanisha  kwamba wao wamejitoa  kuwa na uwezekano huo wa kufanya mazungumzo, kutokana na kuombwa na rais, nan siyo kwamba wanataka sifa , bali mazungumzo hayo ynawezekana tu iwapo sehemu zote mbili zinakubaliana kupokea hata wale walio na tofauti na mawazo yao.

 

12 September 2018, 13:27