Tafuta

Maaskofu wa Malawi watoa onyo viongozi wa serikali na kisiasa  kuacha tabia ya kutumia Kiongozi wa Kanisa kwa manufaa ya siasa zao Maaskofu wa Malawi watoa onyo viongozi wa serikali na kisiasa kuacha tabia ya kutumia Kiongozi wa Kanisa kwa manufaa ya siasa zao 

Malawi:Maaskofu wameonya kutotumia jina la Papa katika siasa!

Maaskofu Katoliki wa Malawi wanashutumu juu ya viongozi wa serikali kutumia Jina la Kiongozi Mkuu wa Kanisa kwa manufaa ya siasa zao.Ni katika uthibitisho wa Barua yao iliyotolewa tarehe 13 Septemba 2018, ambapo maaskofu wakilaana vikali juu taarifa za mjumbe wa chama cha serikali aliyosema wakati wa mkutano huko Blantyre, tarehe 9 Septemba 2018

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baraza la Maaskofu Katoliki wa Malawi wanaawalika viongozi wa Kisiasa wawe, wa serikali na wale wa upinzani kuacha tabia ya kuutumia jina la Baba Mtakatifu katika hali na matumizi yao ya kisiasa. Na kwamba Mashambulizi dhidi ya Baba Mtakatifu Francisko ni shambulio la Kanisa lote ambalo ni Moja,Takatifu, Katoliki na la Mtume

Ni katika uthibitisho wa Barua yao iliyotolewa tarehe 13 Septemba 2018, ambapo maaskofu wakilaana vikali juu taarifa za mjumbe wa chama cha serikali aliyosema wakati wa mkutano huko Blantyre, tarehe 9 Septemba, kwa mujibu wa Rais wa sasa wa Malawi mwenye umri wa miaka 79 Arthur Peter Mutharika, kwamba “ataacha utawala wake,  iwapo Papa Francisko ataacha shughuli yake, kwa maana yeye kama  kiongozi wa Malawi ni kijana zaidi”.

Katika taarifa yao, Maaskofu Katoliki pia wanashutumu mashambulizi ya hivi karibuni juu ya Kanisa Katoliki na mateso ya waamini wake kwa nia ya kupata faida chini ya kivuli cha  mambo ya kisiasa.

Maaskofu wanahakikishia kuwa, kama wachungaji wa Kanisa, wanafahamu wajibu wao wa kukuza umoja na upendo kati ya watu, wakikumbusha kwamba daima wamekuwa  wakishirikiana na imani zote zilizopo nchini kwa kufuata mazungumzo ya kidini, kukuza mema sheria ya kawaida na haki ya  sheria, kwa kuheshimu  haki na hadhi za binadamu

Kutokana na hilo  waraka wa Maaskofu wa Malawi unawaalika wazalendo wa Malawi kutosabambaza habari za kugushi kwa njia ya vyombo vya habari ili kutoendelea kusambaza chuki na mitafaruku  ambayo inaharibu mahusinao mazuri kwa wale ambao wanafikiria tofauti katika maoni ya kisiasa. Kadhalika wametoa wito kwa wote ili kuhakikisha kwamba uelewa wa pamoja na heshima, uvumilivu na ushirikiano wa amani vinadumu kati ya watu wa kila dini nchini Malawi, na hiyo ikiwa ni kwa manufaa ya wazalendao wake wote!

19 September 2018, 15:57