Cerca

Vatican News
Askofu Mkuu Louis Raphael I Kiongozi mkuu wa Kanisa  nchini Iraq Askofu Mkuu Louis Raphael I Kiongozi mkuu wa Kanisa nchini Iraq  (AFP or licensors)

Kanisa la wakaldayo:hakuna maeneo yenye ulinzi kwa wakristo!

Patriki wa Wakaldayo Louis Raphael Sako alisema:Sisi ni sehemu ya Iraq na hatutaki mgawanyiko na uanzishaji wa mikoa maalumu ya madhehebu katika nchi hii. Kardinali Sako anaongeza kusema, sio rahisi kwa Wakristo wa Iraq kuyakimbia mashambulizi ya kihistoria au kutegemeana na unyanyasaji wa mataifa ya nje na silaha.

Frt. Tito Kimario – Vatican

Mwaka huu karibu familia 8,000 za Kikristo ambazo zimeweza kurudi katika vijiji vyao jimbo la Ninawi kaskazini mwa Iraq. Familia zilikimbia mwaka 2014 kutokana na mapigano ya wanamgambo wa kijihadi wa kile kinachojiita Serikali ya kiislam. Hata hivyo leo Kanisa la Wakaldayo halitaki kuanzisha eneo lenye ulinzi kwa Wakristo katika tambarare ya Ninawi.

Katika mahojiano hivi karibuni yaliyotolewa kwenye, gazeti la Kiarabu lililoko London, Patriki wa Wakadayo  Louis Raphael Sako alisema: "Sisi ni sehemu ya Iraq na hatutaki mgawanyiko na uanzishaji wa mikoa maalumu ya madhehebu katika nchi hii ". Kardinali Sako anaongeza kuwa, sio rahisi kwa Wakristo wa Iraq kuyakimbia mashambulizi ya kihistoria au kutegemeana na unyanyasaji wa mataifa  ya nje na silaha.  Hali ya jamii za Kikristo na Kiislamu, Patriaki anathibitisha kuwa bado ni ngumu na inakabiliwa na matukio ya ubaguzi kisiasa na kijamii, na kwa hali yoyote uhamiaji sio suluhisho na Magharibi sio mbinguni.

Mkoa wa Ninawi uliopo kaskazini mwa Iraq, umejaa miji na vijiji vya Wakristo wengi. Kati ya masika na kiangazi 2014 ulikuwa unakaliwa na majihadi  wa Daesh. Katika miezi hiyo, makumi ya maelfu ya wakristo wa Iraq walikimbia vijiji vyake, wakijikinga katika mkoa wa uhuru wa Kurdistan ya Iraq, wakati wengine walikimbilia nchi jirani.

Ndoto ya zamani ya kujenga eneo la kujitegemea kwa wakristo huko Ninawi, bado ipo katika baadhi ya Wakaldayo na Waashuri wa kutoka ugenini, iliyozindua pia na Mkutano wa Kitaifa wa Baraza la Maendeleo mjini Washington kunako mwezi  Septemba 2016, ambaoulikuwa na mada : 'Jinsi ya kuhifadhi Ukristo katika Mashariki ya Kati.

Hata hivyo mwezi Mei 2017, kulifanyika maombi rasmi ya kubadilisha Ninawi kuwa eneo huru na  kuwekwa chini ya ulinzi wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, kulinda, kutatua migogoro na kulinda haki za jamii za Kikristo katika nchi zile ambazo wana mizizi yao. Ni tamko lililokuwa limeelekezwa kwa viongozi wa mkoa na kitaifa na mashirika ya kimataifa kutoka kwa maaskofu wakuu wawili wa Mosul nchini Irak  Askofu Mkuu, Boutros Moshe na Tues Nicodemus Daud Matti Sharaf pamoja Askofu Mar Timotheos Musa al Shamany, wa  Bartellah. Katika kauli mbiu hiyo haki ya kujitawala kwa ajili ya jamii ya Kikristo huko Ninawi imesizitizwa ili kuepuka mapitio ya wanamgambo wa kijihad.

04 September 2018, 16:03