Tafuta

Maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani huko Panama, kwa kutanguliwa na kutangazwa kwa Askofu Romero kuwa Mtakatifu siku zijazo Maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani huko Panama, kwa kutanguliwa na kutangazwa kwa Askofu Romero kuwa Mtakatifu siku zijazo 

Kanisa la Panama lina mengi ya kutoa kwa mahujaji mfano ukarimu!

Kanisa la Panama na Amerika ya Kati lina mengi ya kutoa kwa wageni mahujaji kwa mfano ukarimu, furaha na imani. Wanaweza pia kushuhudia kwa vijana ambao wanatoka mabara tofauti historia ya Kanisa la Amerika ya Kati na Kusini. Kanisa ambalo pia limewahi kuteseka na kushuhudia wafiadini, kwa maana hiyo linajivunia askofu Óscar Arnulfo Romero

Frt. Titus Kimario - Vatican

Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Panama itakuwa fursa ya upyaisho wa imani kwa wote Amerika ya Kati. Hayo yamethibitishwa na Askofu mkuu wa Panama, José Domingo Ulloa Mendieta. Pamoja na ujumbe wa Siku ya Vijana duniani wa Kanisa na Serikali ya Panama, alikutana na wakuu wa idara ya mawasiliano  ya Vatican na kumzawadia  msimamizi, Paolo Ruffini, msalaba wa siku ya vijana duniani. Katika mahojiano hayo na Vatican News, Askofu UIloa aliwashirikisha kwanza moyo ambao watu wa Panama, hasa vijana, walionao kumsubiri Papa Francisko na vijana wa dunia nzima wanaokuja Amerika ya Kati Januari katika siku ya vijana duniani,  ya tatu kwa Papa Francisko.

Maandalizi kupamba moto Panama kwa Siku ya Vijana 2019

Sisi watu wa Panama tunajiandaa kwa mambo mawili makubwa. Kwanza kabisa, tunafungua milango ya nyumba zetu ili familia zetu ziweze kuishi uzoefu wa kumjua Yesu kupitia kwa wageni hawa. Tunaandaa pamoja na mambo mengine miundombinu yote ya kuwakaribisha maelfu na maelfu ya mahujaji  kutoka nchi zaidi ya 190 kutoka katika mabarai 5. Hata hivyo, nadhani jambo muhimu zaidi  tangu kutangazwa kwa siku ya vijana duniani, tunajitayarisha wenyewe kiroho kwa kuishi na kukutana na Yesu na majibu yetu jinsi tulivyo kama Kanisa na nini tunaweza kutoa kwa ndugu wengi ambao watajumuika pamoja Panama wakati wa siku ya vijana duniani.

Matarajio makubwa ni kwamba watajitajirisha kiroho na wakati huo huo watawastawisha pia ndugu wengi watakaokuja. Kile tunachokiishi katika matarajio haya ya furaha ni uwezo wa kushirikikishana mawazo ya jumla, ndoto moja, na kuona kwamba inawezekana kuendelea kuota ndoto mpya na Kanisa jipya! Tunaweka msisitizo mkubwa juu ya mambo ya umoja kati yetu na vijana na tumeamua nguzo tatu: kuwa na uwezo wa kugundua umuhimu wa kuhifadhi na kutunza Nyumba ya pamoja, Uwepo kwa Maria katika maisha yetu na ufahamu wa kuelewa kile ambacho Mungu anamuitia kila mmoja wetu.

Kanisa la Panama lina mengi ya kutoa kwa mahujaji mfano ukarimu

Kanisa la Panama na Amerika ya Kati lina mengi ya kutoa kwa wageni mahujaji kwa mfano ukarimu, furaha na imani. Tunaweza pia kushuhudia kwa vijana ambao wanatoka mabara tofauti historia ya Kanisa la Amerika ya Kati. Kanisa ambalo pia limewahi kuteseka na kushuhudia wafiadini na kwamba linajivunia askofu Óscar Arnulfo Romero, ambaye atatangazwa mtakatifu kunako tarehe 14 Oktoba 2018 pamoja na watatifu wengine 6 akiwawemo hata Mwenyeheri Papa Paulo VI, Askofu Romero ni  mfiadini ambaye sio tu El Salvador au Amerika ya Kati, lakini ni mfano kwa Kanisa zima la ulimwengu.

Kanisa la Cuba limefunga rekodi kwa ushiriki wa vijana 400 watakao udhuria Siku ya Vijana Panama 2019

Wakati huo huo taarifa kutoka Kisiwani Cuba zinasema kuwa vijana 400 wataudhuria Siku ya Vijana duniani huko panama kuanza 22-27 Januari 2019. Kwa upande wa Kanisa la Cuba ni jambo kubwa la aina yake, Kwani vijana kwa mara ya kwanza wataweza kushirikishana urafiki na uzoefu. Yote hayo ni shukrani kwa ushuhuda wa Injili kutoka kwa vijana wenzao  wa dunia yote.

Katika taarifa iliyotolewa na Kamati ya mipango Maandalizi ya Kanisa la Cuba wanasema kuwa vijana  hao wamekwisha anza maandalizi ya tukio la Kanisa, tangu mwezi Oktoba na Novemba 2017, walipofika na hija ya Msalaba katika nchi yao na Picha ya Bikira Maria ambayo ni ishala ya Siku ya Vijana Duniani.

Hata hivyo Askofu Álvaro Veira, wa Tume ya Maaskofu ya kifuchungaji kwa vijana wa Cuba akizungumza na waandishi wa habari , ameeleza kuhusu mafaniko ya  vijana  kuwa wengi kiasi hichoo cha watakao shiriki siku hiyo , ya kwamba wamepata kuongezeka kutokana na shughuli nyeti ya uinjilishaji wa Kanisa la Cuba

 

 

08 September 2018, 08:38