Tafuta

Nembo ya  Ziara ya Papa Franicisko nchini Lithuania Nembo ya Ziara ya Papa Franicisko nchini Lithuania  

Ujumbe wa Maaskofu wa Lithuania kabla ya ziara ya Papa!

Maaskofu wa Lithuania wameandika ujumbe kwa waamini na wenye mapenzi mema siku chache kabla ya ziara ya Papa Francisko mjini Vilniuz tarehe 22 Septemba. Katika ujumbe wao, wanahamasisha kumpokea kwa shauku kubwa kwa maana ni tukio la namna yake kufikiwa na kiongozi maalum wa namna hiyo!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ziara ya Papa Francisko katika nchi yetu ni muhimu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya imani na matumaini na kuimarisha msingi wa jamii ya kidemokrasia. Ndiyo kiini cha maandiko yaliyomo katika waraka wa Maaskofu wa Lithuania katika ujumbe wao kabla ya ziara ya Papa Francisko mjini Vilniuz tarehe 22 Septemba.

Mkutano wa kihistoria katika nchi ndogo kama ile ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II 1993

Maaskofu katika waraka wao wanaandika kuwa: "Kama  ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1993  ilivyogeuka kuwa tukio kubwa la nchi ya Lithuania, ambayo imezaliwa, na  sasa nchi inajiandaa katika mkutano mwingine wa kihistoria.  Kwa mana hiyo ni sababu tatu za ziara hii : kwanza ni zawadi ya kushangaza ya Mungu ambaye katika nchi yetu ndogo inampokea mgeni maalum; kusikiliza neno lake ambalo litaongeza imani yetu na matumaini katika huduma ya bure ya Mungu;tatu na  dunia yote itazungumza nchi yetu na kile ambacho bila shaka kinaweza kuwavutia mahujaji na watalii wengi kututembelea.

Ni fursa maalum ya muungano

Kadhalika maaskofu katoliki nchini Lithuania wanasisitiza kuwa kutokana na kwamba hakuna uwezekano kupata tiketi katika matukio hayo na hivyo wanawaalika watu wasikate tamaa na kupkea fursa ya kumwona papa wakati akipitia barabara za Vilnius na Kaunas, kwa maana atawabariki wota wanakaotoka katika nyumba zao ili kukutana naye njiani.

Kufika kwake pia utakuwa ni fursa maalum ya muungani, na fursa ya kufanya uzoefu mpya wambao ni roho ya kuzaliwa upya kwa miaka 100 iliyopita, wakati wa kupta uhuru , uzoefu wa kushirikishana na nchi nyingine za kibaltiki. Kwa maana hyo maaskofu wanahitimisha waraka wao  wakiwaalika waamini na wenye mapenzi memna kujitoa sadaka yao wenyewa kwa wengine ambayo ndiyo mchuchumalio wa imani na furaha ya umoja wa taifa lao.

07 September 2018, 09:21