Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko akipokea vipaji Baba Mtakatifu Francisko akipokea vipaji 

Wiki ya familia kitaifa nchini Brazil kuanzia 12-18 Agosti 2018

Injili ya familia, furaha ya ulimwengu ndiyo mada ambayo hufanyika kila mwaka katika Jumapili ya pili ya mwezi Agosti, sambamba na sikukuu ya Baba nchini Brazil ikiwa ni wiki ya kitaifa.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Injili ya familia, furaha ya ulimwengu ndiyo mada ya Wiki ya Familia kitaifa katika Kanisa la Brazil ambayo kwa mwaka huu inaanza tarehe 12 hadi 18 Agosti 2018. Ni wiki iliyo andaliwa na Tume ya Baraza la maaskofu kitengo cha maisha na familia pamoja na Tume ya Kitaifa kichungaji kwa ajili  ya shughuli za familia. Tukio hili lina kauli mbiu inayofanana na ile ya  mkutano wa tisa wa dunia  wa familia , mkutano unao tarajiwa kufanyika mjini Dublin nchini Ireland kuanzia tarehe 22-26 Agosti na Baba Mtakatifu anatarajiwa kuudhuria siku mbili za mwisho yaani 25-26 Agosti 2018. 

Familia ni zawadi ya Mungu na tunu kwa ajili ya ulimwengu

Akielezea juu ya mada hiyo  Askofu João Bosco Barbosa de Sousa, wa jimbo la Osasco nchini Brazil na rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu kwa uhamasishaji wa  wiki hiyo amesisitizia upande chanya wa familia  kwamba ni habari njema, wema na zawadi ya Mungu. Askofu pia amesema kwamba familia haitazami tu mafundisho ya Kanisa, wakristo au watawa kwa maana uhakika wa  uwepo wa familia ni furaha ya ulimwengu,  na kukumbusha kuwa, kiini cha familia ni tunu ya binadamu kamili!

Kuongeza nguvu  katika  matendo ya uinjilishaji wa familia 

Katika mtazamo wa mkutano wa Dunia wa Familia huko Dublin Ireland, ni mategemeo ya Askofu Bosco kwamba  mkutano huo unaweza kuongeza juhudi katika   matendo ya kazi za uinjilishaji wa familia  na ametoa  wito wa umakini katika ulimwengu juu ya umuhimu wa familia. Familia imejengwa kwa mujibu wa matashi ya Mungu,  ni kwa njia hiyo tu inaweza kuwa furaha ya ulimwengu amehitimisha.

Safari ya kuelekea Dublin

Hata hivyo wawakilishi wa Mkutano wa dunia wa Familia nchini Ireland,  kutoka  nchini Brazil watakuwepo  familia nyingi ambazo zimejadikisha katika tukio hili akiwemo pia Askofu mwenyewe Bosco , Rais wa Tume ya kitaifa ya Familia , Padre Jorge Alves Filho na waratibu wawili Luiz Zilfredo Stolf e Carmen Rodrigues Stolf.

 

 

12 August 2018, 11:36