Msamaha wa wafungwa 800 nchini Ivory Coast Msamaha wa wafungwa 800 nchini Ivory Coast 

Watu 800 wapewa msamaha wa rais nchini Ivory Coast !

Kwaniaba ya Maaskofu wa Avory Coast Mwenyekiti wa Tume ya Kichungaji jamii wa Kanisa Katolik,i anatoa shukrani za dhati kwa Kiongozi wa Serikali katika maamuzi ya kutoa msamaha wa wafungwa 800. Huu ni mchango mkubwa wa msamaha na mapatano yenye matumaini, ni kama ishara nyingine za mapatano kwa upande wa Rais.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maaskofu wa Ivory Coast wanapokea kwa furaha kubwa ya kihistoria kutokana na Rais wa Jamhuri ya nchi hiyo kutoa msamaha wa watu 800. Huu ni mchango mkubwa wa msamaha na mapatano. Yote hayo ni muhimu katika ujenzi thabiti wa maendeleo na ustawi wa watu na taifa kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na Askofu Antoine Kone askofu wa Jimbo la Odienne na Rais wa Tume ya Baraza la maaskofu, kitengo cha Kichungaji jamii.

Kwa niaba ya maaskofu wakuu na maskofu, anaandika, kama Rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu  katika kitengo cha kichungaji jamii wa Kanisa Katoliki la Ivory Coast, ninapenda kutoa shukrani za dhati kwa Kiongozi wa Serikali katika maamuzi hayo yanayoleta matumaini. Hayo ni matumaini na ishara nyingine za mapatano kwa upande wa Rais.

Pamoja na hayo anawaalika wote waliopokea msamaha huo, waupokee kindugu na kusikiliza, ili kujenga roho ya kizalendo, kwa ajili ya kudumisha amani mioyoni mwao na kuponyesha majeraha ya hali halisi ya jamii kisiasa. Kwa namna hiyo anaongeza, wanaweza kuimarisha kwa dhati amani na kuongeza nguvu ya mapatano kijamii kwa ajili ya umoja wa nchi ya Ivory Coast!

Taarifa zaidi juu ya msamaha huo ni kwamba miongoni mwa watu waliotangazwa kunufaika na msamaha huo wa rais yumo mke wa rais wa  zamani Laurent Gbagbo  Bi Somone Gbagbo . Msamaha huo unatolewa  katika siku kuu ya uhuru wa Ivory Coast ambayo inasherehekewa Agosti 7. Bi Simone Gbagbo alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kufutia machafuko yaliotokea nchini humo na kupelekea rais wa zamani wa nchi hiyo kuondolewa madarakani na kukamatwa. Taarifa hiyo ilitolewa katika hotuba  iliotolewa na rais Ouattara  Jumatatu. Bi Simone Gbagbo alikamatwa na kuhukumiwa Aprili mwaka 2011 na kuhukumiwa  adhabu ya  kifungo cha miaka 25.

Ouattara ametangaza uamuzi huo katika hotuba aliyotoa kwa njia ya televisheni katika utaratibu wa jadi aliojiwekea sambamba na kukaribia maadhimisho ya uhuru wa Ivory Coast. Amesema amesaini msamaha huo ambao unajumuisha wafungwa wapatao 800 wakiwemo wale waliohukumiwa kwa makosa yanayohusiana na mgogoro uliozuka nchini humo baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na yale ya masuala ya usalama yanayohusiana na kipindi cha kuingia kwake madarakani mnamo Mei 21 2011.

Katika hotuba yake hiyo, Rais wa Ivory Coast ametangaza msamaha kwa Simone Gbagbo, mke wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, waziri wa zamani wa ulinzi Lida Kouassi ambaye ni muitifaki mkuu wa Gbagbo na ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mapema mwaka huu kwa kula njama na waziri wa zamani wa ujenzi Assoa Adou ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela mwaka uliopita wa 2017.

23 August 2018, 16:59