Vatican News
Picha ya Mama itapelekwa Panama katika Siku ya Vijana duniani 2019 Picha ya Mama itapelekwa Panama katika Siku ya Vijana duniani 2019  

Picha ya kwanza ya Mama yetu wa Fatima itapelekwa Panama 2019!

Picha ya kwanza ya mama yetu wa Fatima itapelekwa huko Panama katika Mkutano wa Vijana dunia 2019 na itakuwapo katika mikutano miwili msingi : mkesha wa Jumamosi na Jumapili katika Ibada Kuu Takatifu ya Misa kwa mujibu wa maelezo ya Askofu José Domingo Ulloa Mendieta.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika Siku ya Vijana duniani, inayotarajiwa kufanyika mnamo mwaka 2019 huko Panama, kutakuwapo na Picha ya kwanza ya Mama Yetu wa Fatima , ambayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 itatoka nchini Ureno. Aliyetangaza hayo ni Askofu José Domingo Ulloa Mendieta kwa njia ya video, iliyotangazwa katika mchakato wa mkutano na vyombo vya habari, kwa mujibu wa Gazeti Katoliki la Sir.

Historia ya picha hii, ilitengenezwa kwa mujibu wa maelekezo ya Sr. Lucia mnamo mwaka 1947. Ni jambo maalum kwani  mara baada hija kwa mika 64 katika nchi, wakuu vya Madhabahu walikuwa wameamua kuwa ibaki katika madhabahi hiyo bila kuzunguka. Uamuzi huu muhimu umetolewa katika tukio la uhusiano wa Mtakatifu Yohane Paulo II , aliye anzisha Siku ya Vijana duniani. Yeye binafsi alikuwa na ibada kuu huko Fatima kama vile jinsi ilivyo hata kwa kina kwa waamini wa Panama.

Ikumbukwe siku ya Vijana duniani itafanyika kuanzia tarehe 22 -27 Januari 2019. Picha ya Mama yetu wa Fatima itahifadhiwa katika Kanisa la Lourdes  na baadaye kupelekwa huko Parque  ya Perdon katika Kikanisa kidogo cha Ekaristi Takatifu, mahali ambao watailinda na kukesha watawa wa mama Teresa wa Kolkata. Jumamosi na Jumapili itawakilishwa tena katika Mkesha na Misa kuu ya hitimisho ya Siku ya Vijana duniani, itakayo adhimishwa na Baba Mtakatifu Francisko.

 

29 August 2018, 10:44