Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu wa jimbo la Morelia nchini Mexico atoa rambi rambi kufuatia kwa mauaji mengine ya padre mmoja Askofu Mkuu wa jimbo la Morelia nchini Mexico atoa rambi rambi kufuatia kwa mauaji mengine ya padre mmoja  (ANSA)

Padre mwingine nchini Mexico auwawa!

Padre Miguel Gerardo Flores Hernandez alikuwa mzaliwa wa Sombrerete nchini Mexico na alikuwa mmisionari wa Familia Takatifu.Mauti yamemfikia Jumamosi tarehe 25 Agosti 2018 katika mji wa mpya wa manispaa ya Múgica, jimbo Michoacán nchini Mexico.

Frt. Tito Kimaria - Vatican 

Jumamosi  tarehe 25 Agosti 2018 mwili wa mmisionari mmoja ulipatikana katika sehemu isiyoishi watu katika mji wa mpya wa manispaa ya Múgica, jimbo Michoacán nchini Mexico. Kwa mujibu wa shirika la habari za kimisionari Fides, Padre alikuwa amepotea tangu Agosti 18 na siku chache baadaye malalamiko rasmi yaliwasilishwa kwa mamlaka. Kwa mujibu wa askofu msaidizi wa Morelia, askofu Herculano Medina Garfias, mauaji ya Padre labda yalitokana na wizi wa gari lake. Mauaji hayawezi kuwa na uhusiano na uhalifu uliopangwa, lakini uchunguzi unaendelea.

Akiwahimiza waamini na mapadre kuwa waangalifu, Askofu Garfias alisema kuwa katika nyakati kama hizi, kila mtu anajua anaweza kukumbwa na kadhia ya unyanyasaji, wizi, vitisho au unyang’anyi. Msimamo wa Kanisa, anaendelea askofu "Ni kuendeleza kusisitiza upatanisho na msamaha".

Taarifa ya jimbo kuu la Morelia, inatoa pole za rambirambi kutoka kwa Askofu Mkuu, maaskofu wasaidizi, mapadre na jimbo kuu zima: "Mama yetu, Maria wa afya ya wagonjwa, amuombee Padre  wetu. Awape faraja na imani kwa Mama yake, ndugu, jamaa, marafiki na jumuiya nzima ya wamisionari wa Familia takatifu. Tunaendelea kusali kwa ajili ya hali mbaya ya vurugu katika jamii yetu, na Mama Maria atusaidie kumuiga Mwanawe na atusaidie kuishi katika amani yake ".

Padre Miguel Gerardo Flores Hernandez alikuwa mzaliwa wa Sombrerete na alikuwa mmisionari wa Familia Takatifu. Mnamo mwaka 2007 alipewa daraja la upadre na kwa sasa alikuwa paroko msaidizi wa parokia ya Mtakatifu Catarina wa  Alejandria huko Jucutacato. Pia alihudumia Kituo cha Nazareth kwa Mafunzo ya Familia, ambako alifanya kazi na wanandoa, watoto waliotelekezwa na vijana. Alipendwa sana na watu kwa kazi yake nzuri na bila kuchoka kwa ajili ya wengine.

Mauaji ya Padre Flores Hernandes sio suala jipya. Vurugu dhidi ya mapadre zinaendelea kuenea nchini Mexico. Tunakumbuka tukio la Juan Miguel Contreras Garcìa, ambaye aliuawa miezi michache iliyopita na komandoo mmoja katika parokia ya Mtakatifu Pio wa Pietrelcina huko Tlajomulc mara bada ya kuadhimisha  Misa Takatifu. Hata Padre Contreras na wengine wengi waligusa hatima yao. Kwa mujibu wa takwimu za kituo cha  vyombo vya habari katoliki, kuna mapadre  23 waliouawa nchini Mexico wakati wa hawamu ya urais wa miaka sita ya  Enrique Peña Nieto. Mbali na mapadre, tabaka lililoathirika zaidi ni la waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu. Kutokana na hali ilivyo mbaya, Kanisa linaomba sio tu kuweka silaha chini, lakini pia chuki, kisasi na hisia zote za uharibifu; Pia mamlaka imeombwa kutoa mwanga juu ya kile kinachotokea

29 August 2018, 14:29