Tafuta

Vatican News
 Madhabahu ya Mama Maria wa Knock nchini Ireland, mahali ambapo Papa ataitembelea tarehe 26 Agosti 2018 Madhabahu ya Mama Maria wa Knock nchini Ireland, mahali ambapo Papa ataitembelea tarehe 26 Agosti 2018 

Kuanza kwa Novena ya Bikira Maria wa Knock - Ireland

Tema ya toleo la Novena kwa mwaka 2018 ya Mama Maria wa Knock ni Imani na Familia, tema ambayo ina uhusiano na Mkutano wa IX wa Familia duniani mjini Dublin. Papa Francisko atatembelea Madhabahu hiyo ya Kitaifa ya Mama Maria wakati wa ziara yake kwa fursa ya Maadhimisho ya Familia duniani!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Tarehe 14 Agosti 2018 imeanza Novena ya Bikira Maria wa Knoc nchini Ireland. Tema ya toleo la mwaka 2018 ya novena, ni Imani na Familia, tema yenye uhusiano na Mkutano wa IX wa Familia duniani mjini Dublin. Papa Francisko atatembelea Madhabahu hiyo ya Kitaifa ya  Mama Maria huko Knock tarehe 26 Agosti 2018.

Siku ya Jumapili asubuhi tarehe 26 Agosti Papa atakapotembelea madhabahu ya Mama  Maria wa Knock , atakuwa ametimiza ishala yake  kwa milioni ya wazalendo wa Ireland, ambapo kwa kizazi cha muda mrefu karibu nusu karne wamekuwa wakielekea huko. Moyo wa Maria kwa wakatoliki wa nchi ya Ireland unadunda kwa nguvu katika mji mdogo huo ulioko Kaskazini mashariki ya Kisiwa katika ukanda wa Conte wa Mayo. Ni eneo ambalo pia linasimamiwa na msimamizi wa nchi ya Ireland, Mtakatifu Patrick!

Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alikuwa wa kwanza kufungua Sinodi ya kwanza ya Familia, hivyo wa kwanza kuanzisha tukio hili wakati wa utume wake ambapo hata kuandika waraka wake juu ya maisha ya familia akisema: “Maisha ya binadamu yanapitia njia ya familia. Familia ni msingi wa utakatifu. Watoto kamwe hawaatacha ukweli wa familia, wanaweza kuacha nyumba, kuacha mji hata nchi yao lakini hawewezi kamwe kuiacha familia zao. Shule zetu zinaweza kuwa na walimu wanao ofundisha watoto wetu vizuri, lakini sehemu kubwa ya kuishi maisha yao daima ni katika familia zao, yaani wazazi, babu ba bibi zao. Maisha yetu yanajengwa juu ya uhusiano tulio nao na familia zetu, kwa kutupatia msaada na kujenga juu ya furaha ya upendo”.

Ili kuweza kujia zaidia unaweza pia kujitafutia habari zaidi kwa kutumia mtandao ulioandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani kwa Mwaka 2018 kwa anuani ifuatayo: worldmeeting2018.ie. Maandalizi haya yanafamywa kwa ushirikiano kati ya Baraza la Maaskofu Katoliki Ireland na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha ambalo liko chini ya uongozi wa Kardinali Kevin Farrella Mayo.

Historia fupi ya Madhabahu ya Mama Maria wa  Knock nchini Ireland.

Mama Maria waliwatokea waamini 15 wa nchi ya Ireland wenye umri tofauti. Ilikuwa tarehe 21 Agosti 1879 wakati mvua  kubwa zinanyesha katika kijiji. Watu 15 kuanzia umri kati ya miaka 6-75 waliweza kuona Bikira Maria katika picha nyenyekevu kwenye Kikanisa cha Parokia. Kando ya Bikira Maria walionekana picha nyingine ya Mtakatifu Yosefu na Mtakatifu Yohane mwinjili. Kwa mujibu wa utamaduni, wale walioona tukio hilo walibaki  kimya wakisali chini ya mvua kwa masaa mawili lakini bila kulowa nguo zao walizokuwa wamevaa na wakati picha hizo za watu zilikuwa kimya kabla ya  kutoweka. Mchoro wa picha inayowakilisha tukio hili unapatika  katika Madhabahu mpya ya mama Maria wa  Knock, ikionekana jinsi gani watu hao wako mkao wa maono ya watu hao watatu.

Imani ya watu wa Ireland inatiwa nguvu na sala na mapokeo ya mama Maria.

Baada ya siku chache ya tukio hilo lilitingisha nchi yote ya Ireland, viongozi wa Kanisa walichagua tume ambayo iweze kufanya utafiti na kukusanya ushuhuda.Mwanzo wa maajabu ya historia ya Knock umeweza kujotokeza zaidi mara baada ya ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II  manmo mwaka  1979, ambapo katika ziara yake ya kitume ilionekana nusu milioni ya watu na pia kuongezeka matuki mengine mengi hadi sasa.

Kwa muda mfupi baada ya kujitokeza Maria, mji wa Knock umekuwa kituo cha hija  kubwa kwa wazelendo na wenye mapenzi mema kutoka Ireland nzima ,  hata duniani, lakini zaidi  kila mwaka wanakusanyika zaidi ya milioni moja na nusu wakitembelea madhabau hiyo. Vilevile ni  Madhabau inayopendwa sana kutokana kipindi cha kihistoria cha nchi ya Ireland, kwani ilikuwa mwezi Agosti mwaka 1940,  wananchi 50,000 wa Ireland waliudhuria hija kwa ajili ya kuomba amani kwa ajili ya dunia na nchi yenyewe ya Ireland. Mwaka 1954 katika fursa ya Mwaka wa Maria uliotangazwa na Papa Pio XII, zaidi ya mahujaji milioni moja walelekea katika madhabahu ya Knock kwa utashi wa Papa na kuweka taji katika picha ya Mama Maria.

Madhabahu mpoya ilijengwa kwa juhudiu za Monsiyo James Horan.

Baada ya miaka 100 tangu kutokea kwa mama Maria, madhabahu mpya ilijengwa kwa kuongezea katika Kikanisa kidogo. Jiwe la Msingi lilibarikiwa mnamo mwaka 1973 na aliyekuwa awe Baba Mtakatifu, Mwenye heri Papa Paulo VI na kuzinduliwa miaka 6 baadaye yaani  tarehe 18 Julai 1979.  Ni jambo lenye maana kubwa, kwa  jengo hili kusimamishwa kwa misingi 32  inayowakilisha  wafalme 32 wa nchi ya Ireland.  Zaidi jengo hilo ndani yake katikati  kuna zaidi ya vikanisa vidogo, ambavyo vimetolewa kwa ajili ya mama Yetu wa Knock, Mtakatifu Yosefu, Mtakatifu Yohane Mwinjili, Moyo Mtakatifu wa Yesu  na Mtakatifu Colombano.

Maendeleo ya Kanisa kama moyo wa Maria kwa nchi ya Ireland pia inabidi kumtolea shukrani aliyekuwa Paroko  Madhabahu huo Padre Horan  kuanzia mwaka 1967 hadi 1986. Yeye pamoja na kujulikana kuwa ni mjenzi wa Knock  pia kuona madhabahu katika mtindo wa kisasa, pia sifa nyingine ni ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Knock kinachowezesha ndege kutoa kwa urahisi wakati za ziara.

Bikira Maria wa Knock ni moyo wa wahamiaji wa Ireland.

“Kila mara  kwa yoyote anayekwenda hija katika eneo hilo , mahali ambapo zamani ilikuwa ni kijiji cha mbali katika maeneo ya Conte wa Mayo, kila mtu, mwanamke au mtoto anayekuja katika Kanisa la zamani alipotokea Bikira Maria au katika Madhabahu mpya ya Malkia wa Ireland, alisema Karol Woytla, yaani Mtakatifu Yohane Paulo II tarehe 30 Septemba 1979 wakati wa ziara yake ya kitume kwamba, anakuja kupyaisha imani katika wokovu ambao unakuja kwa njia ya Yesu  ambao alibadili sisi sote watoto wa Mungu na warithi wa ufalme wa Mungu. Imani ya watoto wa Ireland  mahujaji kutoka kila pande za dunia imepekelea kwake hata picha ya Knock Muire yaani yaani Kilima cha Maria, ambaye anasimamia nchi ya Ireland na kila mahali popte walipo!

16 August 2018, 09:14