Tafuta

ITALY-ACCIDENT-BRIDGE ITALY-ACCIDENT-BRIDGE 

Kardinali Bagnasco aongoza Ibada ya Mazishi kwa waathirika wa daraja

Kufuatia na janga la kuanguka kwa daraja Morandi huko Genova nchini Italia, misa ya maziko, imefanyika kitaifa kwa ajili ya marehemu wote, iliyoongozwa na Kardinali Angelo Bagnasco Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Genova na kuudhuliwa na mamia elfu ya waamini, viongozi wa serikali na Kanisa, siku ya Jumamosi 18 Agosti 2018.

Sr.Angela Rwezaula - Vatican.

Katika mahubiri yake, Kardinali Bagnasco amesema, kuanguka kwa daraja la Morandi katika maporomoko ya Polcevera, umesababisha kupasuka kwa moyo wa Genova, jeraha ambalo ni lenye kina, na   ambalo limetangeneza uchungu mkubwa kwa wale ambao wamepoteza wanasubiri kupata wapendwa wao ambao bado hawajapatikana, waliopoteza maisha, majeruhi, kwa ajili ya familia zao na wengine wengi ambao bado hawana mahali pa kukaa na hata walioguswa na janga hili kwa ujumla.

Ishara ni nyingi sana za vilio lakini hata ukaribu wa watu wengi tu kwa upande wa lakini  pia hata sehemu mbalimbali za dunia. Kwa pamoja na sala ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye Ijumaa jioni Kardinali anaongeza kuthibitisha kuwa aliwapigia simu ya upendo ili kutaka kuwaonesha ukaribu wake kwa nyanakti hizi ambazo kila sehemu wanasali sala kwa Mungu kwa ajili ya walioathirika. Na mji wa Genova  sasa uko chini ya mtazamo wa dunia!

Huruma ya Mungu na fraha ya Mungu.

Kardinali Bagnasco akiendelea na mahubiri yake amesema, wamekusanyika kwa pamoja ili kujiweka katika huruma ya Mungu na faraja yake ambayo ni Mungu peke yake tu anaweza kuitoa. Upo utambuzi ya kwamba neno lolote la kibinadamu hata kama ni la wazi ni kitu kidogo mbele ya janga kama hili  na kama kila ina ya ulazima wa kuwapo haki, hauwezi kamwe kufuta na  kurudisha hali hiyo. Hii ni hali ambayo imeweza kugusa kwa kina udhaifu wa hali ya kibinadamu kwa mara nyingine tena. Pamoja na hayo Kardinali anathibitisha  ni pale ambapo upo uzoefu ambao kwa wote wameguswa kwa namna nyingine,na ambao inawezekana kuona angalu uzi mwembamba wa mwanga.

Hiyo nikutokana na kwamba kadri unavyojigundua udhaifu na kujiweka mbele ya mwanga, ndiyo zaidi inajitokeza ile hisia ya kutamani mahusianoi ya kibidamu na ndiyo inakuwa kweli ni ya lazima. Husiano huo si tu wa kifamilia na kirafiki, lakini pia haka ule wa   jamiii ambao iuajitambulisha kuwa ni kiraia na ustaarabu. Mahusino hayo yanayo unganisha yanatakiwa kuaminika na kuwa ya dhati na uhakika. Bila upendo wa kuamini, haiwezekani kuishi kwa pamoja. Ni furaha daima na  urahisi wa uwepo wa wengine ambao wanaruhsu kupeleka mbele maisha na kushirikishana furaha na uchungu, kama vile daraja liwezeshalo kuvuka ule utupu na ndiyo maana kuamini kunasaidia kupitia mambo magumu kwa urahisi au ukavu katika njia ya barabara ardhini.

Yesu anaonesha kuwa tunaweza kuamini Mungu hata kama kuna vizingiti vya kinadamu. Imani kwa hakika inatoa vizingiti hivyo vya giza na kuangaza safari hatua kwa hatua na siku hadi siku. Jibu la maombolezo, hawali ya yote  ni uwepo unaosindikiza na Yesu Kristo msulibiwa na Mama Maria chini ya Masalaba wa Mwana. Hizo  ndizo picha na ishala zaidi zinazo onekana wazi na ambazo Bwana hachi kamwe watu wake  bali yuko mbele yao daima.

Mtazamo kwa Mama Maria aliyepalizwa mbinguni.

Kardinali Bagnasco amehitimisha mahubiri na kusema, Mama Maria aliyepalizwa mbinguni anawaalika kwa kipindi hiki kutazama juu mbinguni kwa Mungu, kisima cha matumaini na imani. Kwa kutazama yeye kutazuia mahangaiko na kwamba wanaweza kutazama kwa ujasiri ulimwengu, maisha na mji wao pendevu Genova. Wanaweza kujitazama na  pia kuwatazama wengine  na kujitambua kuwa wote ni ndugu kwasababu ni watoto wa Baba mmoja bila kuwa na tofauti. Wanaweza kujipyaisha imani kwa pamoja na kushikamana kwa karibu katika masaa hayo na wanaweza kujenga madaraja mapya ili kutembea kwa pamoja.

18 August 2018, 16:03