Cerca

Vatican News
Wahamiaji wakiwa wamesimamishwa bandarini Catania Wahamiaji wakiwa wamesimamishwa bandarini Catania  (ANSA)

Kard. Montenegro:ubinafsi mwingi,autengenezi jumuiya ya Ulaya!

Askofu Mkuu wa Agrigento Kardinali Francisko Montenegro wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya kesi ya Meli Diciotti iliyokuwa imeelea na watu 150 huko Catania amasema kuwa anaamini Ulaya haipo. Ujumla ya ubinafsi mwingi hivi, autengenezi jumuiya. Kuwapatia uzito wengine ili wakabiliane na matatizo siyo suluhisho.

Frt. Tito Kimario - Vatican.

Hivi karibuni watoto 27 walishushwa kwenye boti ya Diciotti, waliochwa kwenye bandari ya Catania katika kisiwa cha Sicilia nchini Italiaa kwa siku 5 na ambapo kulikuwa wahamiaji 150 kutoka Eritrea, Siria, Somalia na Sudan. Katika siku hizo walizokaa hapo bila kushushwa imezaa mzozo mkubwa sana hasa katika suala la afya zao kwani waliotembelea kuchunguza walikuta hali halisi ni mbaya, kwa maana wahamiaji wengi walikuwa ugonjwa wa ngozi, mafua na vikoozi.

Ninaamini Ulaya haipo. Ujumla ya ubinafsi mwingi hivi, autengenezi jumuiya. Kuwapatia uzito wengine ili wakabiliane na matatizo ambayo si kushiriki  wote, siyo njia ya kutafuta suluhisho. Tunajionesha ni jinsi gani Ulaya kidogo ina utofauti na haitaki kutazama hali halisi na kuendelea kutazama mambo yake binafsi. Haya ameyasema Askofu Mkuu wa Agrigento Kardinali Francisko Montenegro wakati akizungumza na vyombo vya habari TG24 juu ya kesi ya Meli Dicioti iliyokuwa imeelea na watu 150 huko Catania

Sielewi siasa inayokubali au inayojifanya kuwa  mkono wa chuma na jumuiya ya Ulaya ambayo ni jumuiya yenye mengi. Ameongeza, nina huzunishwa kuona watu wanatendewa kama vitu, kama mzigo ulioegemezwa juu ya meli, ambao unazidi kuteseka, kwa mana hiyo, ninakuwa na wasiwasi, je wakati endelevu utakuwaje. Iwapo hatuwezi kweli kutafuta namna ya kujenga umoja wa kuishi kibinadamu na hasa makaribisho ambayo yanashirikisha wengine kutoka katika mataifa , na kuruhusu watu wawe na maono ya utulivu. Kwa dhati tutajikuta katika matatizo amethibitisha Kardinali Montenegro.

Wakati huo huo, hali mbaya sana, ameeleza pia Teo Di Piazza, mratibu wa timu ya Madaktari wasio na Mipaka iliyopo kwenye bandari ya Catania: "Wanaokolewa watoto wanaokabiliwa na usumbufu mkubwa kimwili na akili: wengine  pamoja na kuonekana kuwa na chakula cha kutosha, wanayo majeraha makubwa kwa ajili ya kukaa Libya. Hata hivyo  mmoja wao alipoteza uwezo wa kuona kwa sababu ya kuwekwa gizani kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kwenye boti hizo hapakuwapo na  uhakika  usafi na lishe kwa kiwango kinachostahili. Inasadikika kulikuwapo na choo na bafu moja kwa ajili ya watu 150. Wahamiaji wanapaswa kukupokelewa haraka iwezekanavyo!

Uchunguzi wa Mwendesha Mashitaka wa Agrigento unaendelea kuelezea huo ni   utekaji nyara, baada ya onyo la Waziri wa Mambo ya Ndani Salvini, ambaye bado ameshikilia msimamo wake: "badilisheni nchi au waziri," kwa wale wanaoshutumu uamuzi wake kwa maana anaongeza. "Siogopi uingiliaji wa Rais wa Jamhuri na " nipo tayari  kwa mahojiano na waziri mkuu".

Kadhalika wajumbe wa Dhamana ya Taifa ya Haki za Wafungwa wamekuwapo  kwenye meli kwa ajili ya ziara na kuthibitisha hali ambazo wahamiaji wanaishi, na usaidizi. Hayo yamefafanuliwa na  mjumbe kutoka katika mfumo wa kitaifa chini ya Itifaki kwa hiari ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya manyanyaso na mateso ya binadamu  (Opcat), iliyoidhinishwa na Italia

Kituo cha Astalli na Caritas ya Catania pia wameelezea kutoelewana kwa hali ya meli ya Diciotti, wakiomba mamlaka ya Italia kuidhinisha kushushwa haraka kwa wakimbizi, bila kujali mazungumzo yaliyokuwa kati ya Italia, Brussels na Nchi za Mataifa ya ulaya kwa ajili ya wakimbizi hawa. Kanisa la Italia lilikuwa liko tayari milango wazi kuwafungulia wahamiaji hawa ili wapate kupekelewa. Hata Kanisa la Catania limejiunga na sauti nyingi katika siku za hivi karibuni kutokana na hali mbaya ya wahamiaji wa meli ya Diciotti, ili waweze hatimaye kushushwa na baada ya mateso mengi kupata suluhisho kwa hali yao ngumu.

Naye Katibu mkuu wa Jimbo Kuu la Catania Monsinyo Salvatore Genchi amesema, “tunaomba kuwa sababu nyingi zilizotolewa, kwanza utu wa binadamu unapaswa kuwekwa mbele, na kwamba haupaswi kuwa jambo la mwisho katika vipaumbele".

 

27 August 2018, 14:56