Tafuta

Askofu Mkuu Berhaneyesus Demerew Sourphiel, C.M./wa Jimbo Kuu la  Addis Ababa-Etiopia Askofu Mkuu Berhaneyesus Demerew Sourphiel, C.M./wa Jimbo Kuu la Addis Ababa-Etiopia  

Kanisa nchini Ethiopia kufanya ziara yake nchini Ujerumani

Kampeni ya Wiki ya utume wa kimisionari mwaka 2018, itafunguliwa tarehe 16 Septemba 2018 huko Erfurt Ujerumani na kumalizika siku ya Jumapili ya utume wa kimisionari duniani tarehe 28 Oktoba 2018. Kardinali Berhaneyesus, CM Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Addis Ababa ataongoza ujumbe wake wakati wa sherehe za ufunguzi mjini Erfurt

Sr Angela Rwezaula - Vatican.

Kanisa Katoliki la Ethiopia litaweza kutembelea nchini Ujerumani mwezi Septemba na Oktoba 2018. Chama Katoliki cha utume wa kimisionari  cha Ujerumani, kimetoa mwaliko kwa wajumbe wawakilishi, ikiwa  ni sehemu ya  Kampeni ya Wiki ya utume wa kimisionari  mwaka 2018, ambayo itafunguliwa mnamo tarehe 16 Septemba 2018 huko Erfurt na kumalizika  siku ya Jumapili ya utume wa kimisionari duniani tarehe 28 Oktoba 2018. Kardinali Berhaneyesus, CM Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Addis Ababa na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ethiopia ataongoza ujumbe huo wakati wa sherehe za ufunguzi mjini Erfurt.

Baraza la Kipapa la vyama vya kitume, limeandaa Jumapili ya Utume wa kimisionari kwa nchini 100 duniani na makusanyo ya sadaka katika makanisa yote kwa siku hiyo yataweza kusaidia majimbo katoliki maskini 1,000 duniani kote. Kwa kawaida kabla ya Siku ya Jumapili ya Kimisionari, kampeni hiyo katika njia hiyo nchini Ujerumani, imekuwa ikiwaalika  makanisa katoliki  mahalia kutoka nchi mbalimbali ili kuwaonesha na kuwasilimulia  watu wa Ujerumani ni  jinsi gani Bara la Afrika, Asia na Austraria wanaishi ukristo na kitu gani wanaweza kujifunza kutoka kwa mmoja na mwengine, kwa jinsi  hiyo mwaka huu ni zamu ya Kanisa la Ethiopia ambalo  limelikwa kuweza  kushirikisha watu wa Ujerumani historia ya maisha yao ya ukristo.

Taarifa kutoka katika Blog ya Amecea inaripoti kwamba, wajumbe watakao wakilisha Kanisa katoliki la Ethiopia wameundwa na maaskofu kumi na mbili, wapadre, watawa na walei. Na mara baada ya kuudhuria maadhimisho ya ufunguzi wa kampeni hiyo, kikundi hicho huko Erfurt septemba 16 wataweza kwenda katika njia tofauti.  Wakiwa pamoja na kikundi cha kimisionari mahalia nchini Uerumani, wataweza kutembelea  na kuona moja au mbili kati ya  majimbo katoliki 25 ya Ujerumani kwa muda tofauti, ili waweze kukutana na wakristo ambao wanahusika wa Ujerumani kwa kujadiliana na kubadilishana mawazo juu maparokia, mashule, vituo katoliki vya wakimbizi, jamii na vijana.

Kwa mujibu ratiba elekezi ya mpango wa utume wa kimisionari, wanasema aidha kutakuwapo na matukio mengine ya kubadilisha utamaduni.  Hata hivyo, ili kuweza kufanikisha ujio wa wajumbe hawa kutoka Ethiopia, miezi kadhaa iliyopita chama cha kimisionari nchini Uerumani kimeweza kupanua hata habari zaidi kwa watu wa Ujerumani, kutoa zana za kampeni, picha za mabango  au filam kuhusiana na  nchi ya Ethiopia. Vifaa hivyo  kwa sasa  viumegawanya katika Makanisa Katoliki ya Ujerumani. Na  moja ya lengo muhimu pia ni kuhusiana na suala la ukuaji wa kahawa nchini Ethiopia.   Kwa maana hiyo Kampeni ya “Coffe to stay itawawezesha watu wa Ujerumani kujifunza ni kwanini wanashirikiana kipindi cha kawahawa ambayo ina maana kubwa katika utamaduni wa jumuiya ya Ethiopia, somo ambalo wanaweza kujifunza mengi

14 August 2018, 17:07