Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Kora 2014 kukutana na Vijana katika madhabahu ya Solmoe Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Kora 2014 kukutana na Vijana katika madhabahu ya Solmoe 

Imepita miaka minne ya Siku ya Vijana Barani Asia

Tarehe 14 Agosti 2014 akiwa katikati ya vijana kwenye madhabahu ya Solmoe huko Aejeon, Papa Francisko alihutubia kwa kirefu kwa lugha ya kingereza ambapo aliwasihi vijana washuhudie Injili ya matumaini ya maisha na kujikomboa mioyoni mwao dhidi ya adui mwovu ubinafsi, vizingiti na ukosefu wa haki.

Sr.Angela Rwezaula - Vatican 

Tarehe 13 Agosti 2014 Papa Francisko alianza ziara yake ya kitume nchini Korea ya Kusini ikiwa ni katika fursa ya Siku ya  Sita ya Vijana Barani Asia. Katika makutano yake na vijana aliwaalika wasali kwa ajili ya umoja wa Korea mbili na kutengeneza ujana kuwa zawadi ya Yesu katika ulimwengu. Katika matarajio ya Sinodi ya Maaskofu mwezi Oktoba 2018 inayo husu vijana, imani na mang’amuzi ya miito, ebu tupitie mikutano miwili  muhimu ya  Papa Francisko na vijana wa Korea ya Kusini kwa miaka 4 iliyopita lakini pia hata kwa waamini wote wa Kore.

Tarehe 13 Agosti 2014 Papa Francisko aliwasiri katika Bara la Asia kwenye fursa hiyo ya Siku ya Sita ya Vijana wa Asia, wakiongozwa na kauli mbiu: Utukufu wa wafia dini uangaze juu yenu. Mkutano wa Siku ya Vijana uliokuwa unawataka vijana kweli kuwa mashuhuda hai wa Kristo kwa kufuata nyayo za wafia dini barani Asia na katika ulimwengu.

Sala kwa ajili ya muungano wa korea moja.

Tarehe 14 Agosti 2014 akiwa katikati ya vijana kwenye madhabahu ya Solmoe huko Aejeon, Papa Francisko alihutubia kwa kirefu kwa lugha ya kingereza ambapo aliwasihi vijana washuhudie Injili ya matumaini ya maisha na kujikomboa mioyoni mwao dhidi ya adui mwovu wa ubinafsi, vizingiti na ukosefu wa haki. Wakati wa kujibu  majibu ya maswali kwa baadhi ya vijana, kwa lugha ya kitaliano aliweza kutoa mwito wa kusali kwa Mungu  kwa ajili ya muungano wa nchi mbili za Korea kwamba: Bwana, sisi ni familia moja, tusaidie kwa ajili ya umoja. Na si kwamba tuwe washindi na wala wa kushindwa, bali kuwa familia moja tu.

Vijana ni zawadi ya Yesu Kristo  na katika ulimwengu.

Baada ya siku mbili, wakati wa kuhitimisha Siku ya Vijana Barani Asia, katika nyumba ya kifalme huko Haemi, Papa Francisko, katika mahubiri yake, aliwashauri vijana wawe sehemu ya kweli  ya maisha katika jamii. Alisisitiza kwamba, wamwachie nafasi Kristo abadili asili yao ya kawaida katika matumaini ya kikristo, nguvu zao katika karama ya maadili; Utashi wao mwema uwe  katika upendo upeo ambao unatambua kujidasaka! Ni kwa namna hiyo ujana wao utaweza kuwa zawadi ya Yesu katika ulimwengu. Na mwisho ilikuwa ni wito wa kujenga Kanisa zaidi Takatifu, zaidi la kimisionari, nyenyekevu, Kanisa ambalo linatambua kupenda, kuabudu Mungu, kutafuta kutumika maskini zaidi, watu walio na upweke, wagonjwa na waliobaguliwa pembezoni mwa jamii.

Hata hivyo akigusia juu ya utengano wa nchi mbili  Baba Mtakatifu Francisko alisema  mang'amuzi ya Kanisa lao,  yanajidhihirisha kwa namna ya pekee katika mazingira ya historia ya wananchi wa Korea; haya ni mang'amuzi ya utengano na kinzani ambazo zimekuwepo kwa takribani miaka sabini. Mwenyezi Mungu anawaalika waamini na wananchi wa Korea katika ujumla wao kutubu na kumwongokea; kufanya tafakari ya kina kuhusu mchango wao katika ubora wa ujenzi wa Jamii inayojikita katika haki na ubinadamu.

Baba Mtakatifu Francisko pia alisema Yesu anawataka kuamini kwamba, msamaha ni mlango unaowaelekeza watu katika upatanisho. Aliwataka wafuasi wake kujikita katika upatanisho bila kubakiza kinyongo. Aliwasihi  kufanya mabadiliko ya kweli kwa maana ni Bwana  anayewajalia neema ya kutekeleza kazi hii. Msalaba wa Kristo unaonesha ile nguvu ya Mwenyezi Mungu katika kutuliza utengano, kuganga madonda na kujenga tena mahusiano yanayojikita katika upendo wa kidugu.

Aidha waliwataka  waamini nchini Korea kuwa na imani katika nguvu ya Msalaba wa Kristo; kujenga na kuimarisha ari na moyo wa urafiki kati ya Wakristo, waamini wa dini mbali mbali pamoja na watu wenye mapenzi mema nchini humo.  Aliwataka wazidi kusali ili kumwomba Mwenyezi Mungu aweze kuwakirimia fursa za majadiliano, mikutano na moyo wa kutaka kuvuka vikwazo vya kutowajali wengine. Waendeleze ukarimu kwa kuwasaidia maskini pamoja na kutambua kwa mapana zaidi ukweli kwamba, wananchi wote wa Korea ni ndugu na watu wa familia moja.

13 August 2018, 13:41