Maandamano na sanamu  ya mama Maria yakiongozwa na Kardinali  Arlindo Furtado huko Fatima Maandamano na sanamu ya mama Maria yakiongozwa na Kardinali Arlindo Furtado huko Fatima 

Hitimisho la hija kimataifa katika madhabahu ya Maria wa Fatima

Wakati wa mahubiri ya ufunguzi wa hija ya kimataifa huko Fatima inayokwenda sambamba na ufunguzi wa miaka 46 ya Juma la wahamiaji na wakimbizi, Kardinali Gomez Furtado amekumbuka ulazima wa kumpokea mwangine na kufikiria utofauti ni utajiri. Serikali na viongozi wa kisiasa huko Marekani na Ulaya wanapaswa kufungua mioyo yao na akili zao kupata suluhisho la tatizo

Sr Angela Rwezaula - Vatican News

Jumatatu 13 Agosti 2018 imemalizika hija ya kimataifa katika Madhabahu ya Fatima iliyokuwa kuwa na nia kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi. Ni hitimisho lililomalizika kwa maadhimisho ya Ekaristi Takatifu kwa kuongozwa na Kardinali Arlindo Gomes Furtado, Askofu Mkuu wa Santiago wa Green Cape. Ni hija ya 78 ya kimataifa inayofanyika kila mwaka mwezi wa Agosti katika Madhabau ya Mama Maria wa Tafitma. Karibu makundi 23 kutoka nchi 20 wamepata kuhudhuria maadhisho hayo yaliyo kuwa na lengo la kuwatazama wahamiaji na wakimbizi.

Kipeo cha kibidamu kama tishio la wakimbizi.

Wakati wa mkutano na vyombo vya habari kabla ya ufunguzi wa hija, Kardinali D. Antonio Marto Askofu Mkuu wa Leiria - Fatima amesisitizia juu ya kipeo cha kibinadamu cha wakimbizi kwamba limekuwa kweli jeshi la maskini wanaotoka maeneo ya Afrika ya Kaskazini. Kardinali Marto amekumbuka kwamba makumi elfu ya miaka, Afrika imekuwa ikinyonywa na nchi za mashariki, kwa kuibiwa mali za asili na ambapo kwa sasa watawala wa nchi za mashariki wanaendelea kuiweka Bara zima katika hali ya vita vya kudumu, ili iwe rahisi kuendeleza unyonyaji na unyanyaswaji hasa kuendeleza kuchanua kwa biashara ya silaha.

Askofu Askofu Mkuu wa Fatima alitoa tamko dhidi ya tawala za nguzu za mashariki wanaondeleza udektata wao  wakati huo  hawana uwezo wa kulinda haki za watu na  kuendelea kuharibu maisha ya milioni ya maskini wanaolazimika kuacha nchi zao ili wasife kwa njaa , umaskini, au waathirika wa vita. Katika mwanga huo pia Kardinali amesisitiza ya kuwa hawezek kukaa kimya bila kusema lolote.

Utofauti ni utajiri.

Wakati wa mahubiri ya ufunguzi wa hija hiyo inayokwenda sambamba na ufunguzi wa miaka 46 ya Juma la wahamiaji na wakimbizi, Kardinali Gomez Furtado amekumbuka ulazima wa kumpokea mwangine na kufikiria utofauti  ni utajiri. Serikali na viongozi wa kisiasa huko Marekani na Ulaya kwa upande mwingine, wanapaswa kufungua mioyo yao na akili zao kimaadili kwa pamoja ili kupata suluhisho la kudumu la amani na  dhidi ya matatizo makubwa ya wahamiaji.

Kwa mujibu wa Kardinali Gomez Furtado, anasema ni lazima kutazama anayepokelewa na kwamba, kabla ya hapo  kwanza alitaliwa na ukoloni, lakini pia hata yule anayetawala na kusabaisha uhamiaji wa kulazimisha! Kwasasa hatuna haja ya kulaumo yoyote, lakini onyo ni kwamba : waafrika nao wanapaswa kuwa watu wazima wawe watu wa kufikiria na kuwajibika, wawe na msimamo wa kusema “tuhaitaji msaada, lakini msitume chakula ua fedha bali tusaidie katika kuandaa na kuendeleza sekta za kiuchumi"; "tunahitaji watalaam, mafundi, watu ambao wanaweza kusaidia na kuitambua hali halisi ya Afrika kwa ajili ya umoja wa kitaifa , kikanda na bara zima!

Hija ya kimataifa katika madhabahu ya Fatima ina utamaduni wa kihistoria kwa mshikamano na utakatifu kwa maana ilianza mnamo tarehe 13 Agosti 1940.  Tangu wakati huo kila mwaka mahujaji  na wakulima nchini  Ureno na wageni, wakati wa kutoa vipaji wanatoa ngano ambayo baadaye hutumika kutengeneza Ostia kwa ajili ya maadhimisho ya misa katika Madhabahu ya Mama Matia wa Fatima. Kwa mujibu wa takwimu za Madhabahu, mwaka 2017 walitoa 8,215 kg  ya ngano na  530kg  za unga wa ngano  ambazo ziliweza kutengeneza  ostia 37,000.  Sehemu nyingine ya ngano pia imeweze kutolewa kwenyemashirikia yanayo fanya kazi kuwasaidia watu wahitaji.

14 August 2018, 16:20