Tafuta

Vatican News
Mashine ya kuhesabu fedha Mashine ya kuhesabu fedha  (AFP or licensors)

Askofu Mkuu Palmer Buckle atoa wito dhidi ya rushwa

Katika fursa ya kampeni ya mpango wa madhehebu dhidi ya ufisadi, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Cape Coast nchi Ghana ametoa wito kwa wananchi wote wa Ghana kutoa mchango wa ushirikiano wao ili kuweza kupambana na tukio hili.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Rushwa ni janga kubwa ambalo limezidi kuwa sugu na kusambaa kama magonjwa ya kuambukiza katika nchi ya Ghana. Askofu Mkuu Gabriel Charles Palmer-Buckle, Askofu Mkuu wa Cape Coast katika fursa ya kuanzisha mpango huo uitwao, Sema juu yake, pinga na kutoa ripoti za ufisadi, ni moja ya mpango madhubuti ulio anzishwa na  Ghana Integrity Initiative (GII), shirika la kimataifa lisilo la kiserikali kwa ajili ya kuzuia ufisadi na uwazi wa kimataifa. Mpango huo unasaidiwa na Serikali ya Denimark ambao unatazama kuwahusisha viongozi wa kidini na  mashirika ya kidini mahalia katika hali halisi na mpango wa utekelezaji wa  wa Taifa wa  miaka 10 dhidi ya rushwa na ufisadi (Nacap, 2015-2024).

Mada hiyo kwa sasa ipo katika maoni ya umma nchini Ghana.Ni tukio ambalo limekuwa kweli tema nyeti katika moni ya umma nchini Ghana, shukrani kwa waandishi wa habari ambao wanasaidiwa na Anas Aremeyaw Anas ambaye pia ameweza kusimulia historia nyingi  zinazo husiana na vitendo vya rushwa na uhalifu wa kupangwa nchini Ghana. Suala hili pia limeleta matatizo makubwa hasa kitaifa katika nyanja ya mchezo wa mpira kitaifa hadi kufikia mwenyekiti wake kujiudhuru. Kwa mujibu wa ripoti ya umma ya mwaka 2016 zaidi ya asilimia 80% ya wazalendo wa Ghana wanadhibitisha juu ya nchi yao kuelekea katika njia mbaya kwasababu ya rushwa na ufisadi.

Katika hotuba ya Askofu Mkuu Palmer-Buckle anahamasisha wote wajikite kuwa sehemu ya kutafuta suluhisho. Gazeti la Ghana linamkariri akitoa wito kwa wananchi wote wa Ghana kugeuka kuwa sehemu ya kupata suluhisho la tatizo hilo sugu na kuwakumbusha kuwa, rushwa ni kasumba mbaya ya kuhukumiwa na madhehebu yote ya dini kwani  iwapo  hawafanyi kuwa sehemu ya kutafuta  ufumbuzi, ina maana kwamba hajihusishi kuwa  siyo sehemu ya matatizo. Kwa maana hiyo ni muda sasa wa kujiwekea msimamo kimaadili, kiutamaduni katika jamii ya Ghana amethibitisha.

Nafasi msingi ya viongozi wa kidini dhidi ya rushwa. Katika  hotuba ya Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Cape Coast nchini Ghana ameunda mwangu mkuu   hata kwa msemaji wa Maimam mkuu wa waislam nchini Ghana Shehe Aremeyaw Shaibu, ambaye ameonesha jinsi gani rushwa katika taasisi nyingi inaziidi kuondoa matumaini ya wanazalendo kwa wafanyakazi na viongozi wa Serikali.  Balozi wa Danmark nchini Ghana, Tove Tegnbol, akitoa  hotuba wakati wa uzinduzi amesisitizia upande wa nafasi msingi ya viongozi wa kidini ili waweze kuwashawishi wazalendo wa Ghana, wazungumzie juu yake, wasikubali hali hii na kutoe ripoti juu ya matukio haya na hata kuyapinga.

10 August 2018, 11:31