Vatican News
Kanisa kuu la Mtakatifu Francisko huko Assisi Kanisa kuu la Mtakatifu Francisko huko Assisi  

Asisi ni mgeni wa Mkutano wa kwanza wa maombi ya kiekumene!

Mkutano wa kiekumene wa Assisi, kwa wakatoliki unaangukia siku ambayo inadhimishwa Siku ya IV ya Dunia ya Kuombea Huduma ya Viumbe, iliyotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwaka 2015

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa nchi za Ulaya (CCEE) wanafungua maombi kwa ajili ya huduma ya viumbe kuanzia tarehe 1 Septemba hadi tarehe 4 Oktoba 2018, kwa ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa kiekumene mjini Assisi kwa ajili ya maombi ya hduma ya viumbe. Mkutano huo umetayarishwa na Kamati ya kiekumene, ambayo inaunganisha na mipango mbalimbali, kati hizo ni katika dunia wakatoliki ambapo kuna chama kikatoliki cha utetezi wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano wa kiekumene wa Assisi, kwa wakatoliki unaangukia siku ambayo inadhimshwa siku ya IV ya  Dunia ya kuombea huduma kwa viumbe, iliyotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwaka 2015. Itakayo adhimishwa tarehe 1 Septemba 2018 kuugana na Kanisa la Kiorthodox, ambapo katika maadhimisho hayo na mkutano huo kutakuwapo na wawakilishi wachahce wa CCEE anbao wataongozwa na Askofu Mkuu wa Genova, Kardinali Angelo Bagnasco, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya, Askofu Mkuu Angelo Massafra OFM wa jimbo Kuu la Scutari, Pult na Askofu mhusika wa kitengo cha ulinzi na utunzaji wa Mazingira kutoka katika Tume ya CCEE kwaajili ya utume kichungaji wa kijamii.

Kama Kardinali Bagnasco alivyokuwa ametoa wito wake hivi karibuni kwa njia ya video iliyoandaliwa na Baraza la Makanisa Ulaya (KEK), Kardinali katika viedo hiyo alisema, Ekolojia ya mazingira inahitaji ekolojia fungamani na ndiyo maana hata ekolojia ya binadamu inaheshimu hadhi ya kila mtu; maisha na kile chochote ambacho tangu mwanzo wa maisha ya kutungwa mimba hadi kufikia mauti yake ya kawaida, vyote hivyo ni sehemu ya shughuli hiyo ya ekolojia fungamani. Kutokana na hayo yote, wakristo wote na katika mkutano wa Assisi kwa namna ya pekee una maana kubwa ya kutafuta katika mwanga wa imani iliyo moja na uwajibikaji wa pamoja!

31 August 2018, 15:50